Katibu wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Buhalahala mjini Geita
Lazaro Kagoma anatuhumiwa kutafuna kiasi
cha zaidi ya milioni 20 ambazo zilitolewa na halmashauri ya mji wa Geita kwa
kikundi cha wajasiliamali Geita (KIWAGE)walipatiwa na halmashauri ya mji wa
Geita.
Kagoma ambaye ni Katibu wa Kikundi hicho cha KIWAGE anadaiwa
kuwazunguka wanachama wenzake na kutafuna
fedha walizopatiwa kwa ajili
ya manufaa ya kufanya shughuli za ujasiliamali inadaiwa badala yake alizifanyia
matumizi yake binafsi kinyume na matarajio ya kikundi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Shilabela Bw,Elias
Mtoni alisema kikundi hicho kimeonekana
kuwa na ujanja mwingi kutokana na udanganyifu ambao wameweza
kuufanya wa kuidanganya halmashauri ya
mji wa Geita na mwisho wa siku kupatiwa fedha kiasi cha Milioni 45.
Shida Mpondi ambaye ni mkazi wa Geita,ameitaka serikali kufanya
uhakiki kabla ya kutoa mikopo kwenye vikundi kwa maana ya kujildhihirisha na
kujua shughuli ambazo vikundi vinafanya kazi za ujasiriamali ili kuepukana na
utapeli wa namna kama hiyo iliyojitokeza.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola
amekiri kupokea malalamiko dhidi ya kikundi hicho huku akisema kwamba Katibu wa
Kiwage amekuwa akiwatishia wanakikundi wenzake wanapohoji fedha walizokopeshwa.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti amejibu tuhuma za
kuhusihwa na kikundi hicho kuwa ni mmoja wa watu aliyekipigia chepuo ili
kurudisha fadhila katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015 jambo ambalo amesema sio
sahihi kwani fedha hizo wamekuwa wakikopesha kwa vijana na vikundi ambavyo
vimekidhi vigezo pasipo kubagua itikadi ya vyama vya siasa.
Hata hivyo mtandao huu umewatafuta
wahusika akiwemo mwenyekiti na Katibu wa kikundi hicho kwa njia ya simu na simu
zilikuwa zikiita bila majibu huku ofisi
za kiwage zikiwa zimefungwa kwa takribani miezi mitano sasa.
0 comments:
Post a Comment