Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod
Mgimwa akizungumza na viongozi wa kata ya Kibengu kuhusu maswala mbalimbali ya kimaendeleo sambamba na kutoa maagizo mbalimbali ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya kata ya hiyo na jimbo hilo kwa ujumla
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod
Mgimwa na viongozi wengine wakisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya kata ya Kibengu
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod
Mgimwa akiangalia moja ya mradi wa ujenzi wa vyoo
Diwani wa kata ya Kibengu Zakayo Kilyenyi akiwa na viongozi wa kata ya hiyo mara baada ya kutoka kwenye kikao na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini
Na Fredy Mgunda,Mufindi.
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini
amewataka viongozi wa vijiji na kata kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wote
ambao hawataki kuwapele shule watoto wao wakifaulu mitihani ya shule ya msingi
kwenda shule ya sekondari.
Akizungumza na blog hii mbunge Mahamuod
Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi
Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa
viongozi hapo baadae.
“Nasema tena haiwezekani kila
mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini
sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za
kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia
maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa
Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la
Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani
pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo
yao.
“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu
mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana
nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake
wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa
shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa
Aidha Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike
kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na
kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea
kufungwa jela kwa kuwa sheria itachukua mkondo wake.
“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa
“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa
Mgimwa aliwapongeza walimu wa shule za
msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye
mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.
“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa
hii kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua
katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa
kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari ya Ilogombe Pastor Haonga alisema kuwa wazazi wengi wa kata ya Kibengu wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.
“Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi
wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu
kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia
wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema Haonga
Haonga alimuomba mbunge wa jimbo la
Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi wa kata
ya Kibengu ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.
“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi
ni mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa
hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo
inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema
Haonga.
Aidha Mfikwa alisema kuwa wamekuwa
wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada
zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea
kuwa wafanyakazi za ndani tu
Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu
alikiri kuwa wazazi wengi wa kata hiyo
hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya
familia zao na taifa kwa ujumla.
“Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu
wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa
wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda
kuwafanya kazi za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi
Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata
ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya
kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la
kuboresha maisha ya watoto hao.
“Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa
sana katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo
elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi
Nao watendaji wa vijiji vitano vya kata
ya Kibengu ambao ni Dominicus Nyaulingo,Saifod Mwengwa,Haruna Kalenga, Richard
Mandili na Demetus Kanyika walisema kuwa wamepokea agizo la mbunge na
watalifanyia kazi kwa ukamilifu kwa kufuata sheria ili kuhakikisha watoto wa
kata hiyo wanapata elimu kama inavyotakiwa.
Na kata ya Kibengu inajumuisha vijiji
vitano ambavyo ni kijiji cha Kibengu,kijiji cha Igereke,kijiji cha
Ilogombe,kijiji cha Usokami na kijiji cha Kipanga
0 comments:
Post a Comment