Kada wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Michael Mlowe akiwa kwenye moja ya majukwa akikitumikia chama cha mapinduzi kueleza jinsi gani serikalia ya chama hicho inavyotekeleza wajibu wake kwa wananchi.
mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas akiwa jukwaani na diwani mpya wa kata ya Kihesa Jully Sawani.
Na Fredy Mgunda,Iringa
KADA
wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa Michael Mlowe amempongeza mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas kwa
kazi anazizofanya za kuleta maendeleo katika mkoa wa huu.
Akizungumza
na blog Mlowe alisema kuwa Asas amekuwa kiungo mkubwa kwa kuleta maendeleo hasa
ukianga vitu alivyofinya hivi karibuni utajua kuwa jinsi gani amekuwa msaada
kwa wananchi wa Iringa.
“Mimi
naunga mkono juhudi za MNEC kwa kazi zake katika manispaa yetu ya Iringa hata
mkoa mzi amekuwa akitatua changamoto nyingi ambazo hata serikali imeshindwa
kuzitatua hivyo naomba wananchi waendelee kumuunga mkono kazi zake” alisema
Mlowe
Mlowe
alisema kuwa hivi karibu Asas alitoa ahadi kwa wananchi wa kata ya kihesa na
akaanza mara moja kuitekeleza hivyo utagundua kuwa ni mtu wa maendeleo na
anafaida kuwa kwa taifa leo
Ukiangalia
utagundua kuwa mafundi wameanza kufanya shughuli za kimaendeleo za wananchi
kama ilivyokuwa ahadi yake na ya MNEC Asas hivyo muda sio mrefu wananchi
watapata ajira hapa
“Mwandishi
ukiangalia hapa unawaona mafundi wanaendeleoa na kazi hivyo najua baada ya muda
mufupi kila kitu kitakuwa kimemalizika na kuanza kutumika kwa faida ya wananchi
wa kata ya kihesa” alisema Mlowe
Mlowe
alisema kuwa anamshukuru MNEC Salim Asas kwa kutekeleza ahadi alizowahidi
wakazi wa kihesa kwa kuwa tayari ameshatoa mifuko mia mbili (200) ya saruji
katika shule ya sekondari ya Kihesa na tayari mafundi wapo kazini wameanza
kumalizia ujenzi wa jengo la biashara ambalo litaongeza ajira kwa wakazi wa
kata ya Kihesa na nje ya kata hii.
Aidha
Mlowe aliwapongeza wanachama wa chama cha mapinduzi kwa kumchagua Salim Asas
kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwani
wamempata mtu sahihi katika kukikuza chama hicho manispaa ya iringa ambako ndio
kuanaonekana kuna upinzani mkubwa.
“Saizi
chama cha mapinduzi kimempata mtu sahihi kabisa wa kurudisha umoja wa wanachama
na kuongeza wanachama wapya na kuuwa upizani kabisa kwa kuwa alisema kuwa yeye ni
paka hivyo anaweza kufukuza panya wote waliopo manispaa ya Iringa” alisema
Mlowe
Mlowe
amewataka wanachama na wananchi wa mkoa wa Iringa kuendelea kuunga mkono mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas ili
kuleta maendeleo na kuahakikisha Iringa inakuwa jiji kwa kuwa pasipokuwa na
maendeleo ya kutosha Iringa hatuwezi kuwa jiji.
0 comments:
Post a Comment