Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akimweleza mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu namna ambavyo Kituo cha Utafiti Mikocheni kinavyochangia kwenye kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo kushoto kwa Dkt. Mwanjelwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Thomas Kashillilah
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na
mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu katika moja ya maabara
ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na
mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mkuu
wa Idara ya Udhibiti wa Magonjwa ya Mimea Dkt. Deusdeth Mbanzibwa katika moja
ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Aina za mbegu mbalimbali za mihogo ambazo ni Sehemu ya
matokeo ya tafiti zinazoendeshwa na Kituo cha Utafiti Mikocheni ambazo Naibu
Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri
wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu walipata nafasi ya kujionea
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na
mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza
Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya ambaye amewaeleza
faida za mbegu za mahindi ziligunduliwa Kituoni hapo kupitia Mradi wa WEMA
Dkt.
Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Dkt.
Christopher Materu Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Wadudu na Magonjwa kutoka Kituo
cha Utafiti Mikocheni namna nzuri ya kudhiti magonjwa ya mimea kwa kutumia
wadudu marafiki
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa
ameishukuru Serikali ya China kwa kuonyesha nia ya kusaidia eneo la utafiti na
maendeleo hususan kwenye kuendeleza zao la minazi na mihogo kupitia Kituo cha
Utafiti wa Mazao cha Mikocheni JIJINI Dar es Salaam.
Dkt Mwanjelwa amemshukuru Serikali ya China kupitia Naibu
Waziri wa Kilimo wa China Dkt Qu Dongyu mara baada ya kufanya ziara katika
Kituo hicho mapema leo.
Katika Wasilisho lake kwa ugeni wa Waziri huyo wa Kilimo
kutoka China, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti Mikocheni Dkt Fred
Tairo amesema Kituo kimekuwa kikiendesha tafiti mbalimbali zenye lengo la
kuzuia na kukabiliana na magonjwa hatari ya minazi na mihogo lakini kikwazo kikubwa
kimekuwa teknolojia hafifu na uzoefu mdogo katika nyanja hiyo.
Mara baada ya wasilisho hilo Naibu Waziri wa Kilimo wa China
ambaye anataaluma ya kilimo amesema Serikali ya China ipo tayari kuisaidia
Tanzania kwenye maeneo ya utafiti wa kuzuia magonjwa ya mazao kwenye minazi na
mihongo na kutoa wito kwa Watafiti wa Tanzania kuongeza juhudi katika kubunia
teknolojia mbazo zitakuwa rahisi na rafiki kwa Wakulima wa Tanzania ili iwe rahisi
kuziuza na baadae pato lake lisaidie Kituo hicho kujiendesha.
Dkt Qu Dongyu yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali pamoja na Mwenyeji
wake, Dkt Mary Mwanjelwa ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuitembelea
maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni na kujionea matokeo ya tafiti
mbalimbali.
Akizungumzia kuhusu uwezeshaji wa Serikali ya China kwa Kituo
cha Utafiti Mikocheni, Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce
Kulaya amesema kwa sehemu kubwa Kituo kimekuwa kikipata uwezeshaji kutoka Serikalini
pamoja na Wabia wa Maendeleo kama Mfuko wa Bill and Belinda Gates Foundation na
kuongeza kuwa uwezeshaji kama kutoka Serikali ya China utaongeza tija na
uzalishaji katika mazao mengine si kwa minazi na mihogo tu.
Dkt Qu Dongyu anataraji kumaliza ziara yake ya Kiserikali
hapo kesho kwa kukutana na Wawekezaji wa China waishio Tanzania na baadae
atareje nyumbani siku hiyo ya Jumamosi.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment