VIKUNDI nane vya wakulima wa mahindi na
mpunga mkoani Iringa vyenye jumla ya wakulima 857, vimepata mikopo ya Sh Bilioni
1.006 kutoka katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Shughuli ya utiaji saini makubaliano ya
mikopo kati ya benki hiyo na vikundi hivyo ilifanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita katika kijiji cha Igomaa, wilayani Mufundi mkoani Iringa katika hafla
iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mikopo
na Biashara wa benki hiyo Robert Pascal inaonesha vikundi hivyo vinakuwa vya
kwanza kuanza kunufaika na mikopo ya benki hiyo ambayo mpaka sasa inafanya kazi
katika mikoa sita ya Iringa, Njombe, Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam.
Vikundi hivyo na kiasi cha fedha walichopata
ni Idodi Farmers Association chenye wakulima 108 (Sh milioni 119.3), Igomaa
Cooperative Society chenye wakulima 130 (Sh Milioni 180.4), na Kihorogota Cooperative
Society wakulima 85 (Sh Milioni 77.4).
Vingine ni Kilolo Mali Mbichi Amcosi
wakulima 31 (Sh Milioni 53.4), Mgololo Cooperative Society wakulima 87 (Sh
Milioni 132), Mtambula Amcosi wakulima
160 (Sh Milioni 69), Mufindi Cooperative Society wakulima 152 ( Sh Milioni 221)
na usolanga Cooperative Society wakulima 104 (Sh Milioni 124.1).
Pascal alisema vikundi hivyo vimepata
mikopo hiyo baada ya kukidhi vigezo mbalimbali vilivyowekwa na benki hiyo ikiwa
ni pamoja na taarifa za akaunti za benki, barua za maombi, usajili wa kikundi,
mtiririko wa mapato na matumizi, andiko la biashara, katiba, cheti cha ukomo wa madeni, taarifa za
ukaguzi wa fedha na dhamana za mikopo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TADB, Rosebud
Kurwijila alisema tangu bodi ya benki hiyo izinduliwe mwaka 2013, walikuwa
katika maandalizi ya kimkakati ya namna ya kuwafikishia mikopo hiyo wakulima.
“Leo tumeanza, tumetoa mikopo kwa
wakulima nyumbani kwao, yaani benki imewafuata wakulima huko huko walipo
mashambani kwao na kuwapa mikopo, ni jambo la kujivunia sana,” alisema.
Alisema benki hiyo imeanza kazi na
itaendelea kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo nchi nzima, hatua kwa hatua
ikilenga kuwafikia wakulima wengi kwa kadri itakavyowezekana.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Thomas
Samkyi alisema vikundi hivyo ni kati ya vikundi 89 vya wakulima vya mkoani
Iringa walivyovipatia elimu ya jinsi ya kunufaika na mikopo hiyo, Oktoba mwaka
huu.
Alisema mikopo hiyo inayotozwa riba ya
asilimia saba hadi nane inatolewa kwa ajli ya kufanikisha shughuli za kilimo
kwenye minyororo ya thamani katika mazao
ya nafaka (mahindi na mpunga), mifungo
(ng’ombe wa nyama na maziwa na ufugaji wa kuku wa kienyeji), uvivi (samaki), mboga
mboga, matunda, viungo, maua na mazao yanayosindikwa viwandani.
Kwa kupitia mikopo hiyo, Samkyi alisema
wakulima hao watapata pembejeo za uhakika zikiwemo mbegu bora, mbolea na dawa,
vifaa na teknolojia ya umwagiliaji na fedha kwa ajili ya kulipia gharama
mbalimbali za uzalishaji.
Samkyi alisema lengo la benki hiyo ni
kuwafanya wakulima kuondokana na mfumo wa kilimo cha zamani na kufanya
mapinduzi ya kilimo ili kuongeza tija na hatimaye kufikia maendeleo
yanayotokana na mapinduzi hayo.
Naye Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina
Masenza alisema benki hiyo ni mkombozi wa wakulima kwa kuwa benki nyingi nchini
zimekuwa zikijikita kwenye biashara tu na kuacha wakulima wakikosa fursa ya
mikopo na kama wakipata inakuwa ya muda mfupi ikiwa na riba kubwa.
Mmoja wa wanufaika wa mikopo hiyo, Emmanuel Fungo alisema ujio wa benki hiyo ni faraja kwa wakulima hao kwani mbali na kuwawezesha kuongeza tija katika uzalishaji, inawatafutia masoko ya bidhaa wanazozalisha. VIKUNDI nane vya wakulima wa mahindi na mpunga mkoani Iringa vyenye jumla ya wakulima 857, vimepata mikopo ya Sh Bilioni 1.006 kutoka katika Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).
Shughuli ya utiaji saini makubaliano ya
mikopo kati ya benki hiyo na vikundi hivyo ilifanyika mwishoni mwa wiki
iliyopita katika kijiji cha Igomaa, wilayani Mufundi mkoani Iringa katika hafla
iliyohudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mikopo
na Biashara wa benki hiyo Robert Pascal inaonesha vikundi hivyo vinakuwa vya
kwanza kuanza kunufaika na mikopo ya benki hiyo ambayo mpaka sasa inafanya kazi
katika mikoa sita ya Iringa, Njombe, Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam.
Vikundi hivyo na kiasi cha fedha walichopata
ni Idodi Farmers Association chenye wakulima 108 (Sh milioni 119.3), Igomaa
Cooperative Society chenye wakulima 130 (Sh Milioni 180.4), na Kihorogota Cooperative
Society wakulima 85 (Sh Milioni 77.4).
Vingine ni Kilolo Mali Mbichi Amcosi
wakulima 31 (Sh Milioni 53.4), Mgololo Cooperative Society wakulima 87 (Sh
Milioni 132), Mtambula Amcosi wakulima
160 (Sh Milioni 69), Mufindi Cooperative Society wakulima 152 ( Sh Milioni 221)
na usolanga Cooperative Society wakulima 104 (Sh Milioni 124.1).
Pascal alisema vikundi hivyo vimepata
mikopo hiyo baada ya kukidhi vigezo mbalimbali vilivyowekwa na benki hiyo ikiwa
ni pamoja na taarifa za akaunti za benki, barua za maombi, usajili wa kikundi,
mtiririko wa mapato na matumizi, andiko la biashara, katiba, cheti cha ukomo wa madeni, taarifa za
ukaguzi wa fedha na dhamana za mikopo.
Mwenyekiti wa Bodi ya TADB, Rosebud
Kurwijila alisema tangu bodi ya benki hiyo izinduliwe mwaka 2013, walikuwa
katika maandalizi ya kimkakati ya namna ya kuwafikishia mikopo hiyo wakulima.
“Leo tumeanza, tumetoa mikopo kwa
wakulima nyumbani kwao, yaani benki imewafuata wakulima huko huko walipo
mashambani kwao na kuwapa mikopo, ni jambo la kujivunia sana,” alisema.
Alisema benki hiyo imeanza kazi na
itaendelea kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo nchi nzima, hatua kwa hatua
ikilenga kuwafikia wakulima wengi kwa kadri itakavyowezekana.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Thomas
Samkyi alisema vikundi hivyo ni kati ya vikundi 89 vya wakulima vya mkoani
Iringa walivyovipatia elimu ya jinsi ya kunufaika na mikopo hiyo, Oktoba mwaka
huu.
Alisema mikopo hiyo inayotozwa riba ya
asilimia saba hadi nane inatolewa kwa ajli ya kufanikisha shughuli za kilimo
kwenye minyororo ya thamani katika mazao
ya nafaka (mahindi na mpunga), mifungo
(ng’ombe wa nyama na maziwa na ufugaji wa kuku wa kienyeji), uvivi (samaki), mboga
mboga, matunda, viungo, maua na mazao yanayosindikwa viwandani.
Kwa kupitia mikopo hiyo, Samkyi alisema
wakulima hao watapata pembejeo za uhakika zikiwemo mbegu bora, mbolea na dawa,
vifaa na teknolojia ya umwagiliaji na fedha kwa ajili ya kulipia gharama
mbalimbali za uzalishaji.
Samkyi alisema lengo la benki hiyo ni
kuwafanya wakulima kuondokana na mfumo wa kilimo cha zamani na kufanya
mapinduzi ya kilimo ili kuongeza tija na hatimaye kufikia maendeleo
yanayotokana na mapinduzi hayo.
Naye Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina
Masenza alisema benki hiyo ni mkombozi wa wakulima kwa kuwa benki nyingi nchini
zimekuwa zikijikita kwenye biashara tu na kuacha wakulima wakikosa fursa ya
mikopo na kama wakipata inakuwa ya muda mfupi ikiwa na riba kubwa.
Mmoja wa wanufaika wa mikopo hiyo, Emmanuel Fungo alisema ujio wa benki hiyo ni faraja kwa wakulima hao kwani mbali na kuwawezesha kuongeza tija katika uzalishaji, inawatafutia masoko ya bidhaa wanazozalisha.
0 comments:
Post a Comment