Wednesday, January 31, 2018

MBUNGE CHUMI AITAKA SERIKALI KUWAPA VYETI WALIOPOTEZA

Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi ameishauri Serikali kuwapa vyeti au nakala ya vyeti vya kidato cha nne na sita watu ambao kwa namna moja au nyingine walipotelewa na vyeti hivyo.

Chumi alitoa ushauri huo kufuatia majibu ya Serikali kuwa imekuwa vigumu kuwapa vyeti watu waliomaliza masomo kabla ya mwaka 2009 kwa madai kuwa vyeti vya wakati huo havikuwa vinawekwa picha ya mhitimu.

Mbunge huyo alieleza kuwa, ili kuwaondolea usumbufu waliopoteza vyeti, serikali ikishathibitisha kuwa muhusika ndio mtu sahihi, basi apewe japo nakala ya cheti kama wanavyofanya Vyuo Vikuu.

Awali katika swali lake la msingi, Chumi alitaka kufahamu utaratibu unaotumika kwa mtu aliyepoteza cheti na kwanini kumekuwa na ucheleweshaji wa huduma hiyo kwa watu ambao wameomba ajira au nafasi za masomo.


'Unakuta mtu kaomba ajira au nafasi ya kuendelea na masomo, anajaza fomu Baraza la Mitihani ili cheti kitumwe sehemu husika, lakini mara nyingi NECTA wanachelewa kuwasilisha cheti na hivyo kuwakosesha watu nafasi walizoomba' alihoji Chumi na kusisitiza kuwa, wahusika wapewe japo nakala ya cheti.

Akijibu, naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha alisema kuwa NECTA baada ya kupokea maombi huyashughulikia  ndani ya wiki nne kuyatuma yanakohitajika.

'Hata hivyo niseme wazi kuwa hakuna linaloshindikana, Serikali inachukua ushauri wa mbunge na kuona namna bora ya kulishughulikia jambo hili'. Alifafanua Ole Nasha.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na utitiri wa matangazo ya watu waliopotelewa vyeti, lakini pia baadhi ya watu wamekuwa wakihoji kwanini baada ya kujiridhisha, Baraza la Mitihani lisiwape japo nakala za vyeti.

Chumi alisema kuwa, mfumo wa sasa unawakosesha fursa za ajira na nafasi za masomo waliopotelewa vyeti hasa pale NECTA inapochelewa kuwasilisha maombi yao kule kunakohusika.

UWT MANISPAA YA IRINGA WAAZIMISHA MIAKA 41 KWA KUFANYA USAFI NA KUTOA ZAWADI KATIKA KITUO CHA AFYA CHA NGOME

 mwenyekiti wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa Ashura Jongo akiwa na viongozi wengi wameazimisha miaka arobain na moja (41) kwa kufanya usafi katika kituo cha afya cha ngome pamoja na kugawa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa 
 Huyu ni mmoja ya wanawake wa umoja wa chama cha mapinduzi CCM waliokuwa wakitoa zawadi kwenye kituo cha afya cha Ngome kata ya Kihesa manispaa ya Iringa
 Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa wameazimisha miaka arobain na moja (41) kwa kufanya usafi katika kituo cha afya cha ngome pamoja na kugawa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa ambalo wamelazwa katika kituo hicho kwa lengo la kuwafikia na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi
Umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa wameazimisha miaka arobain na moja (41) kwa kufanya usafi katika kituo cha afya cha ngome pamoja na kugawa zawadi mbalimbali

Na Fredy Mgunda,Iringa.

UMOJA wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) manispaa ya Iringa wameazimisha miaka arobain na moja (41) kwa kufanya usafi katika kituo cha afya cha ngome pamoja na kugawa zawadi mbalimbali kwa wagonjwa ambalo wamelazwa katika kituo hicho kwa lengo la kuwafikia na kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

Akizungumza wakati wa kufanya usafi na kugawa zawadi,mwenyekiti wa umoja huo Ashura Jongo alisema kuwa anaishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kufanya kazi kwa kuwafikia wananchi wa chini hasa wale wanyonge kwa kutimiza kile ambacho kilikuwa kimeahidiwa wakati wa kuomba kura za kuongoza nchi.

“Kiukweli naomba nichukue nafasi hii kumpongeza sana  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kwa kuwa anafanya kazi kubwa sana kuhakikisha kuwa Tanzania inapiga hatua ya kimaendeleo hivyo ni lazima tuonge mkono juhudi hizi” alisema Jongo

Jongo alisema kuwa serikali imefanikisha kuleta mabadiliko ya haraka katika sekta ya afya tofauti na hali ilivyokuwa hapo awali hivyo wananchi wanatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa kujituma ili kuunga mkono juhudi hizi.

“Najua kuwa mnaona kwa macho yenu kiasi gani serikali ya wamu ya tano jinsi gani huduma za afya zilivyo boreshwa na lazima tujivunie hiki kinachofanywa na Rais wetu,mimi binafsi naunga mkono juhudi hizi na ninaomba wananchi nao waunge mkono juhudi hizi” alsema Jongo

 Jongo alisema kuwa kuongezaka kwa hospital za rufaa kwenye mikoa,vituo vya afya kwenye kata au tarafa, zahanati kwenye vijiji na mitaa ni hatua kubwa ya kimaendeleo hivyo ndio serikali ya awamu hii inavyotekeleza vilivyo ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020.

“Nyie ni mashaidi kuwa zamani tulikuwa tunaishia kuwa na hospitali za mikoa tu lakini kwa sasa mambo yamebadilika kila kitu kinazidi kuwa kwenye ubora unaostahili kuwahudumia wananchi waliotuweka madarakani” alisema Jongo

Lakini sio afya tu hata ukiangalia saizi tunapata elimu bure ambayo inamwezesha kila mwanafunzi kusoma bure na kuhakikisha tunapunguza wimbi la wanafunzi kukosa elimu ambapo inasaidia kuwa nakizazi cha wasomi hapo baadae.

Naye mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa umoja huo Devota Chaula alisema kuwa wanawake wengi wanakumbuna na changamoto mbalimbali hasa kukosa mikopo midogo midogo hivyo serikali ya awamu ya tano hivyo inatakiwa kuangalia kwa jicho la tatu kutusaidia kupata mikopo hiyo.

“Wanawake wanafanya kazi kwa umoja sana hivyo kukosa mikopo kuasababisha kuduma kwa kipato cha kukuza uchumi wa mtu moja moja na taifa kwa ujumla hivyo ukifanikiwa kumweza mwanamke basi umewawezesha wananchi wote hapa nchi” alisema Chaula

Chaula alisema kuwa watanzania wanatakiwa kubadili kwa kuacha kuishi kimazoea hivyo wanatakiwa kuendana na kasi ya serikali ya awmu ya tano kwa kufanya kazi kwa kujituma ili kukuza vipato vyao.

Kwa upande mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Sezalia Endru aliwashukuru viongozi hao wa umoja wa wanawake wa ccm manispaa ya Iringa kwa kuwatembelea na kufanya usafi na zawadi walizozitoa kwa watumishi na wagonjwa waliokuwepo muda huo.


“Tunaomba mtufikishe salamu kwa Rais wa serikali ya awamu ya tano kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kuboresha sekta ya afya kwa kuwa hali ya sasa kila kitu kinaenda kwa wakati” alisema Endru

MTULIA AZIDI KUITEKA KINONDONI ... SERA ZAKE ZAWA GUMZO


Image may contain: one or more people, people on stage, crowd and outdoor

Mgombea Ubunge katika jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM akinadi ser zake jukwaani na kuomba kura kwa wapiga kura wa Kata ya Ndugumbi.


**********

*YALIYOSEMWA NA MGOMBEA UBUNGE WA CCM JIMBO LA KINONDONI, MAULID SAID MTULIA KWENYE MKUTANO WA KAMPENI KATA YA NDUGUMBI JUMANNE JANUARI 30, 2018*

"Kama Mtulia angekuwa amenunuliwa asingepewa tena dhamana ya kugombea Ubunge " - Mtulia

"Ningekaaje kwenye chama ambacho Mwenyekiti na Katibu hawaelewani, nimejitoa ili niwe na uhuru wa kuwatumikia wana Kinondoni." - Mtulia


"Kile chama hamkusikia kimesimamisha wabunge 8, mlitaka nami nisimamishwe?" - Mtulia

"Mtulia nimejiuzulu ili kuwaokoa Wananchi wa jimbo la Kinondoni" - Mtulia

"Kuhama chama ili kujiunga na chama chenye maendeleo, huo ni usaliti?" - Mtulia

"Mtulia huyu ndio aliotoa hela yake mfukoni kujenga visima vya maji; Mtulia aliyefungua kesi mahakamani kuzuia bomoa bomoa; ndio Mtulia yule aliyeomba maghorofa ya Magomeni Watu waliojitokeza nyumba zao wakae bure" - Mtulia

"Mtulia mimi ni yule yule mkinichagua nitahakikisha naendelea kuwaletea maendeleo nikishirikiana na viongozi wenzangu na Rais wangu mpendwa Di. Magufuli " - Mtulia

"Ninaomba tena ridhaa ili nihakikishe nawaletea maendeleo wana Kinondoni kutokana na kugombea kwenye chama chenye ilani ya uchaguzi iliyoshikan dola" - Mtulia

"Naomba dhamana ya kugombea ili nikashirikiane na wenzangu kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM 2015 - 2020" - Mtulia

"Kazi yangu mkinichagua ni kwenda kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM na si porojo wala usanii" - Mtulia

"Ukichagua Mtulia umechagua maendeleo; ukimchagua Mtulia umejenga daraja kati ya Wananchi na Serikali" - Mtulia

MBUNGE KABATI ATOA MSAADA WA MIFUKO 25 YA SARUJI KATIKA KANISA LA FREE PENTECOST CHURCH OF TANZANIA

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akimkabidhi mchungaji
wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero huku akiwa sambamba na katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa na viongozi mbalimbali  wa chama cha mapinduzi wilaya ya Iringa pamoja na madiwani wa chama hicho.
 Hili ndio kanisa la la Free Pentecost Church of Tanzania ambalo mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati amekabidhi mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati ametoa msaada wa mifuko ishirini na tano (25) katika kanisa la Free Pentecost Church of Tanzania lililopo kata ya Isakalilo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kanisa jipya ili kuendelea kutoa huduma bora ya neon la mungu.

Akizungumza wakati wa ibada iliyofanyika katika kanisani hilo Kabati alisema kuwa ni heri kujibembeleza kwa mwenye mungu kuliko kujipendekeza kwa binadamu mwenzako hivyo ni bora kuchangia shughuli za kihoro kuliko shughuli za kidunia.

“Mimi nimejitoa kuchangia shughuli zote zinazo muhusu mungu hivyo naomba mnishirikishe nami nitakuja bila kusita kwa kuwa ndio kazi yangu hata iliyonifanikisha mimi kuwa mbunge” alisema Kabati

Kabati alisema kuwa aliwaahidi kuwapa mifuko ishirini na tano ya saruji hivyo ametimiza ahadi hiyo kwa kuwapa mifuko ya saruji yote aliyoiadi hivyo amefanikiwa kutekeleza na kuwaomba wananchi wananchi wengine kuchangia maendeleo ya kanisani.

“Alikuja diwani hapa kwa niaba yangu na kuahidi mifuko hiyo ambayo ni sawa na tani moja hivyo nimeamua kutimiza kuwa lengo langu nikiahidi kitu lazima nitimize malengo yangu ya kuitoa ahadi hiyo” alisema Kabati

Aidha Kabati aliwata wananchi na viongozi mbalimbali kuendelea kuchangia shughuli za kimaendeleo kwa jamii na taasisi ambazo hazina uwezo wa kufikia mafanikio yanayotakiwa kwa ajili ya kutatua kero zinazorudisha nyuma maendeleo.

Kabati amesema kuwa wananchi na viongozi wanatakiwa kumtegemea mungu ili kuweza kufanikisha malengo wanayotarajia.

Katika hatua nyingine Kabati amewataka wazazi kuwapeleka shule watoto wao ili wakapate elimu ambayo ndiyo itakuwa dira ya maisha yao ya baadae.

Kwa uoande wake mchungaji wa kanisa hilo la Free Pentecost Church of Tanzania Francis Okero alisema kuwa walikuja viongozi wengi na kutoa ahadi nyingi lakini hakuna hata mmoja aliyetimiza ahadi yake zaidi ya mbunge Ritta Kabati.

"Nilialika wageni wengi wakala na kutoa ahadi nyingi kwa mbwembwe nyingi lakini kilichotokea hadi sana viongozi wote hakuna aliyetimiza malengo hayo hivyo nichukue furasa kushukuru" alisema Okero

Mchungaji Okero alimshukuru mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake ambayo itatusaidia katika ujenzi wa kanisa letu

Tuesday, January 30, 2018

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA TRIONI MOJA KUTOKA GLOBAL FUND KUSAIDIA TB,UKIMWI NA MALARIA


 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora (kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban, wakisaini hati za makabidhiano ya sh. trioni moja zilizotolewa na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia mapambano ya Ukimwi, TB na Malaria katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo. Wengine waliosimama katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  na viongozi wengine kutoka Global Fund.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika hafla hiyo.

Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mnufaika wa Global Fund, Joan akielezea jinsi alivyo nufaika na shirika hilo.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine, akizungumza.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban (kulia), akimkabidhi hati ya makabidhiano Mwakilishi wa Global Fund Tanzania, Linden Morrison.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora, akizungumza.
Taswira ya ukumbi wa mkutano katika uzinduzi huo.


Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Kimataifa la Global Fund limetoa shilingi trioni moja kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya mapambano ya magonjwa ya ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa mwaka 2018-2020. 

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makabidhiano ya fedha hizo baina ya mfuko huo na serikali Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema fedha hizo ni muhimu sana kwa nchi yetu.

Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kupambana na magonjwa hayo ambapo kwa ugonjwa wa ukimwi zimetolewa sh.bilioni 769, TB sh. bilioni 67 wakati malaria sh.bilioni 320.

Alisema fedha hizo zitatumika kikamilifu kwa lengo lililokusudiwa na zitasimamiwa  na Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Afya na Mashirika Yasiyo ya kiserikali.

Alisema katika masuala ya ukimwi zitatumika kwa ajili ya vipimo, dawa za kurefusha maisha na kufubaza virusi kwa wagonjwa wa ukimwi na katika ugonjwa wa malaria fedha hizo zitatumika kwa ajili ya vipimo na matibabu pamoja na kununua vyandarua.


"Kwa upande wa wagonjwa wa TB ni asilimia 40 tu ndio waliofika kwenye vituo vya afya na kuthibitika kuwa na maambukizi na wamepatiwa matibabu lakini tunataka hadi ifikapo mwaka 2020 tunataka asilimia 70 ya watanzania watakaogundulika kuwa na maambukizi wajulikane na wapatiwe matibabu" alisema Ummy.

Ummy aliongeza kuwa kati ya wagonjwa 100 wenye maambukizi ya TB wagonjwa 90 waliothibitika kuwa na maambukizi walitibiwa na kupona kabisa.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka Katibu Mkuu wa Wizara yake, Tamisemi na Ofisi ya Rais kuhakikisha wanazisimamia vizuri fedha hizo ili kupata matokeo mazuri waliyo yakusudia.

Mratibu wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya Tanzania (TANPUD), Happy Assan alisema mradi huo utawasaidia sana na kuhakikisha hawataathirika ukizingatia kuwa fedha hizo zitawafikia walengwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine alisema mradi Global Fund imewasaidia waathirika 900,000 kwa kuwapa dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARV na kufubaza virusi vya ugonjwa huo.



Monday, January 29, 2018

DKT. MWANJELWA AISHUKURU CHINA KWA KUONYESHA NIA YA KUISAIDIA TANZANIA KWENYE MAENDELEO YA TAFITI ZA KILIMO CHA MINAZI NA MIHOGO

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akimweleza mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu namna ambavyo Kituo cha Utafiti Mikocheni kinavyochangia kwenye kuongeza tija na uzalishaji katika Sekta ya Kilimo kushoto kwa Dkt. Mwanjelwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt. Thomas Kashillilah
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Magonjwa ya Mimea Dkt. Deusdeth Mbanzibwa katika moja ya maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni
Aina za mbegu mbalimbali za mihogo ambazo ni Sehemu ya matokeo ya tafiti zinazoendeshwa na Kituo cha Utafiti Mikocheni ambazo Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu walipata nafasi ya kujionea
Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Naibu Waziri wa Kilimo wa China, Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya ambaye amewaeleza faida za mbegu za mahindi ziligunduliwa Kituoni hapo kupitia Mradi wa WEMA
Dkt. Mary Mwanjelwa akiwa na mgeni wake Dkt. Qu Dongyu wakimsikiliza Dkt. Christopher Materu Mkuu wa Idara ya Udhibiti wa Wadudu na Magonjwa kutoka Kituo cha Utafiti Mikocheni namna nzuri ya kudhiti magonjwa ya mimea kwa kutumia wadudu marafiki

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuonyesha nia ya kusaidia eneo la utafiti na maendeleo hususan kwenye kuendeleza zao la minazi na mihogo kupitia Kituo cha Utafiti wa Mazao cha Mikocheni JIJINI Dar es Salaam.

Dkt Mwanjelwa amemshukuru Serikali ya China kupitia Naibu Waziri wa Kilimo wa China Dkt Qu Dongyu mara baada ya kufanya ziara katika Kituo hicho mapema leo.

Katika Wasilisho lake kwa ugeni wa Waziri huyo wa Kilimo kutoka China, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Utafiti Mikocheni Dkt Fred Tairo amesema Kituo kimekuwa kikiendesha tafiti mbalimbali zenye lengo la kuzuia na kukabiliana na magonjwa hatari ya minazi na mihogo lakini kikwazo kikubwa kimekuwa teknolojia hafifu na uzoefu mdogo katika nyanja hiyo.

Mara baada ya wasilisho hilo Naibu Waziri wa Kilimo wa China ambaye anataaluma ya kilimo amesema Serikali ya China ipo tayari kuisaidia Tanzania kwenye maeneo ya utafiti wa kuzuia magonjwa ya mazao kwenye minazi na mihongo na kutoa wito kwa Watafiti wa Tanzania kuongeza juhudi katika kubunia teknolojia mbazo zitakuwa rahisi na rafiki kwa Wakulima wa Tanzania ili iwe rahisi kuziuza na baadae pato lake lisaidie Kituo hicho kujiendesha.

Dkt Qu Dongyu yupo nchini kwa ziara ya Kiserikali pamoja na Mwenyeji wake, Dkt Mary Mwanjelwa ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuitembelea maabara ya Kituo cha Utafiti Mikocheni na kujionea matokeo ya tafiti mbalimbali.

Akizungumzia kuhusu uwezeshaji wa Serikali ya China kwa Kituo cha Utafiti Mikocheni, Mtafiti Mwandamizi wa Kituo cha Mikocheni Dkt Aloyce Kulaya amesema kwa sehemu kubwa Kituo kimekuwa kikipata uwezeshaji kutoka Serikalini pamoja na Wabia wa Maendeleo kama Mfuko wa Bill and Belinda Gates Foundation na kuongeza kuwa uwezeshaji kama kutoka Serikali ya China utaongeza tija na uzalishaji katika mazao mengine si kwa minazi na mihogo tu.

Dkt Qu Dongyu anataraji kumaliza ziara yake ya Kiserikali hapo kesho kwa kukutana na Wawekezaji wa China waishio Tanzania na baadae atareje nyumbani siku hiyo ya Jumamosi.

MWISHO.

MWANAUME ATUHUMIWA KUMUUA MKE NA MTOTO WAKE WILAYANI CHATO


Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye eneo ambalo kumetokea tukio.

Jirani wa Familia ambapo kumetokea mauaji Bi,Mariam Shija akizungumza na waandishi wa habari kwa masikitiko juu ya tukio hilo.
Diwani wa Kata  Minkoto   , Bw Geroge Magezi akiwasisitiza wananchi kushiriana na jeshi la Polisi kwenye suala la ulinzi na usalama.

Dk Masanja Mchanganya anayetokea kituo cha afya cha Bwanga akielezea namna ambavyo wamebaini mwili wa marehemu majeraha yaliyopo baada ya kufanya uchunguzi.


Na,Joel Maduka,Chato.

Mkazi wa kijiji cha Minkoto Wilaya ya Chato Mkoani Geita Bw Hoja Kasumbakabo ( 25) anatuhumiwa kumuua mke wake Spensioza Petro (22) kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali mwilini na kisha kumnyonga mtoto Brison Hoja mwenye umri wa miezi mitatu kisha   kutokomea kusikojulikana.

Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw Leo Nkwabi amesema tukio hilo limetokea tarehe 24 mwezi januari kuamkia tarehe 25 kwenye kijiji hicho ambapo ilibainika miili kuonekana chini ya Sakafu ndani ya chumba walichokuwa wanaishi huku mwili wa mwanamke huyo ukiwa na majeraha sehemu ya kooni, mgongoni na tumboni huku utumbo ukiwa nje.

Mzazi wa marehemu Mzee Petro Lusaga ameelezea kusikitisha na tukio hilo na kwamba hakuwahai kuwaona marehemu na mumewe wakiwa na ugomvi kwani kwa kipindi chote walikuwa wakiishi  kwa amani bila ya kuwa na malumbano wala kelele zozote ndani ya familia yao.

Bi,Judy Masanja ambaye ni jirani wa karibu wa familia hiyo alisema na yeye ameshangazwa na kifo hicho kwani hawakuwai kuwa na ugomvi na siku hiyo walikuwa wamekaa nje na walikuwa wakizungumza vizuri tu hivyo hata  yeye kifo kimekuacha na maswali mengi ya kujiuliza.

Kwa upande wake Diwani wa Kata hiyo, Bw Geroge Magezi amewataka wananchi  kuimarisha ulinzi na kuisaidia serikali kumtafuta mtuhumiwa huku akisisitiza wanaume kuacha mauaji ya namna hiyo.

Dr Masanja Mchanganya anayetokea kituo cha afya cha Bwanga amethibitisha tukio hilo ambapo katika uchunguzi walioufanya wamegundua kuwa marehemu alikuwa na majerahaa matatu makubwa 


KATIBU WA CCM KATA YA BUHALAHALA ATUHUMIWA KUTAFUNA KIASI CHA SH MILIONI 20

Ofisi za  kikundi cha wajasiliamali (KIWAGE) zilizopo mtaa wa Shilabela Mjini Geita  zikiwa zimefungwa .

Mwenyekiti wa Mtaa wa Shilabela   Bw,Elias  Mtoni akielezea suala la vikundi ambavyo vimeonekana kuwa na dhana ya utapeli juu ya fedha za wajalisiamali .

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola akizungumza juu ya uwepo wa taarifa za kiongozi ambaye analalamikiwa kutokomea na fedha za wajasiliamali.
Na,Joel Maduka,Geita...


Katibu wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Buhalahala mjini Geita Lazaro Kagoma  anatuhumiwa kutafuna kiasi cha zaidi ya milioni 20 ambazo  zilitolewa na halmashauri ya mji wa Geita kwa kikundi cha wajasiliamali Geita (KIWAGE)walipatiwa na halmashauri ya mji wa Geita.


Kagoma ambaye ni Katibu wa Kikundi hicho cha KIWAGE anadaiwa kuwazunguka wanachama wenzake na kutafuna   fedha walizopatiwa  kwa ajili ya manufaa ya kufanya shughuli za ujasiliamali inadaiwa badala yake alizifanyia matumizi yake binafsi kinyume na matarajio ya kikundi.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Shilabela  Bw,Elias Mtoni  alisema  kikundi hicho kimeonekana kuwa na  ujanja  mwingi kutokana na udanganyifu ambao wameweza kuufanya wa kuidanganya halmashauri  ya mji wa Geita na mwisho wa siku kupatiwa fedha  kiasi cha  Milioni 45.

Shida Mpondi ambaye ni mkazi wa Geita,ameitaka serikali kufanya uhakiki kabla ya kutoa mikopo kwenye vikundi kwa maana ya kujildhihirisha na kujua shughuli ambazo vikundi vinafanya kazi za ujasiriamali ili kuepukana na utapeli wa namna kama hiyo iliyojitokeza.


Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita Leonard Bugomola amekiri kupokea malalamiko dhidi ya kikundi hicho huku akisema kwamba Katibu wa Kiwage amekuwa akiwatishia wanakikundi wenzake wanapohoji fedha walizokopeshwa.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti amejibu  tuhuma za kuhusihwa na kikundi hicho kuwa ni mmoja wa watu aliyekipigia chepuo ili kurudisha fadhila katika uchaguzi Mkuu mwaka 2015 jambo ambalo amesema sio sahihi kwani fedha hizo wamekuwa wakikopesha kwa vijana na vikundi ambavyo vimekidhi vigezo pasipo kubagua itikadi ya vyama vya siasa.


Hata hivyo mtandao huu  umewatafuta wahusika akiwemo mwenyekiti na Katibu wa kikundi hicho kwa njia ya simu na simu zilikuwa zikiita bila majibu  huku ofisi za kiwage zikiwa zimefungwa kwa takribani miezi mitano sasa. 

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More