Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka
hiyo,Salum Shamte kulia akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martine Shigella walioipata mamlaka hiyo ushindi wa kuwa mamlaka
bora ya huduma za maji na usafi wa mazingira nchini mwaka 2014/2015
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka
hiyo,Salum Shamte kulia akimkabidhi tuzo hiyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)Mhandisi Joshua
Mgeyekwa anayeshuhudia katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine
Shigella.
Mkuu wa Tanga,Martine Shigella akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) uliyoteuliwa na Waziri wa Maji |
Mkuu wa Tanga,Martine Shigella
akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya mamlaka ya Maji
Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) uliyoteuliwa na Waziri wa Maji
ikiwemo wafanyakazi wa Mamlaka hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga akiwa
kwenye picha ya pamoja na mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maji na Usafi
wa Mazingira Jijini Tanga ( Tanga Uwasa) na wafanyakazi wa mamlaka hiyo
MKUU wa Kitengo cha Uzalishaji
Maji katika kituo cha Kusafishia Maji
Mabayani Jijini Tanga,Faraji Nyoni akimueleza mkuu wa Mkoa wa
Tanga,Martine Shigella namna uzalishaji wa maji uzalishaji unavyofanyika
na usafishaji wake kabla ya kuwafikia wananchi.
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa
Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) imeweza kuwa mamlaka ya kwanza
nchini kufikia vigezo vya kupewa leseni ya EWURA ya Daraja la kwanza
(Class 1Lesence).
Leseni hiyo ilitolewa Juni 17
mwaka huu na Waziri wa Maji na Umwagiliaji katika mkutano wa kuzindua
ripoti ya mwaka 2014/2015 ya mamlaka za maji uliofanyika Mjini
Dodoma.
Akizungumza mwishoni mwa
wiki,Mkurugenzi Mkuu wa EWURA ,Felix Ngamlagosi alisema kuwa leseni
hiyo ilitolewa kwa Tanga Uwasa na kwa sasa ndio mamlaka ya maji pekee
nchini iliyo na leseni ya EWURA ya daraja la kwanza nchini.
Alisema kuwa leseni hiyo ya daraja
la kwanza imetolewa baada ya EWURA kupitia utendaji kazi wa Tanga Uwasa
na kutadhimini viwango vilivyowekwa ili mamlaka ya maji kuweza kupata
daraja la kwanza na kujiridhisha kuwa vimefikiwa.
Aidha alisema vigezo ambavyo
vimeangaliwa kuwa mamkala bora ni kugharamia uendeshaji wa
mamlaka,kugharamia uchakavu wa miundombinu na kuweza kulipia riba za
mikopo ya uwekezaji.
"Lakini pia uwezo wa
Mamlaka hiyo kujitegemea kiufundi na
kiuendeshaji"
Mkurugenzi huyo alisema kuwa
mamlaka hiyo imeweza kuwa ya kwanza kwa miaka mitatu mfululizo miongoni
mwa mamlaka kubwa 25 za maji zinazotoa huduma katika makao makuu ya
mikoa Tanzania bara.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Tanga (Tanga Uwasa)
Mhandisi Joshua Mgeyekwa alisema wao kama mamlaka wataendelea
kuhakikisha wanatoa huduma bora zinazoendena na viwango vikubwa ili
kuendelea kuwa mamlaka bora nchini.
Alisema pamoja na changamoto
walizokuwa nazo lakini wameweka mikakati kabambe ya kuhakikisha
wanakabiliana nazo kwa kuwawezesha wananchi waweze kunufaika ana huduma
ya Maji kwa kiwango kikubwa .
"Lakini pia sisi kama mamlaka
tumejiwekea mipango kabambe ya kuhakikisha huduma za maji zinaimarika
sambamba na kujiandaa na fursa ya ujio wa bomba la mafuta utakaoanzia
nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga ili changamoto ya maji isiwepo
wakati wa ujio wa fursa hiyo.
habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
0 comments:
Post a Comment