UMOJA
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema Rais John Magufuli,
hana baya alilolitamka katika mikutano yake ya Unguja na Pemba, bali
amezika upotoshaji wa siasa uchwara, kusafisha upepo mchafu na kufumba
vinywa vya wanasiasa wakorofi na wazushi.
Pia
umetoa mwito kwa Wazanzibari kwa nguvu zote kupinga siasa chafu au
zenye lengo la kuwagawa, kuwatenganisha au kuwahasimisha badala yake
watambue umuhimu wa kuendeleza umoja, amani na maendeleo ya kiuchumi na
kijamii.
Kaimu
Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alisema hayo ofisini kwake
Makao Makuu ya CCM, Dodoma, alipotakiwa kueleza maoni yake kuhusu
shutuma anazotupiwa Rais Magufuli ikidaiwa na baadhi ya wanasiasa kwamba
alilenga kuamsha joto la mtafaruku wa kisiasa visiwani humo.
Shaka
alisema hotuba ya Rais Dk Magufuli imezima siasa za uzushi na dhidi ya
viongozi wanaowadanganya wafuasi wao kwamba utafanyika Uchaguzi Mkuu
mwingine kabla ya mwaka 2020 na Rais Ali Mohamed Shein ataondoka
madarakani ili kumpisha Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.
Shaka
alisema hotuba ya Rais ilikuwa yenye mashiko na maudhui, makatazo,
maonyo, maelezo na wosia uliojiegemeza katika kudumisha amani nchini.
“Kuhubiri
amani ni dhamana yake kiutawala, kuwaonya wananchi wanaokata mikarafuu,
kutoboa mitumbwi, kufyeka mazao mashambani na wengine kukataa kuwauzia
bidhaa wenzao halikuwa kosa na si jambo baya kama inavyoelezwa na
wazushi wa kisiasa,” alisema Shaka.
Aidha,
alisema ikiwa kuna mwanasiasa asiyemtii Rais aliye madarakani Zanzibar
na hata kukataa hata mkono wake, hakuna sababu kwa kiongozi huyo kutaka
msaada kwenye serikali asiyoitambua.
“Iweje
baniani mbaya kiatu chake dawa, unajigamba humtambui Rais aliyeshinda
na kuunda serikali ila unadoea fedha zinazokusanywa na serikali
usioitambua ili usaidiwe na kulipwa marupurupu. UVCCM inaunga mkono SMZ
kumnyima stahili zote hadi atakaipomtambua Rais,” alisema Shaka.
Kaimu
Katibu Mkuu huyo alisema wakati wa utawala wa Dk Salmin Amour Juma,
Maalim Seif aliposema hamtambui kama mshindi halali hakuwa akilipwa
chochote, Rais mstaafu Amani Abeid Karume hakumlipa kitu hadi
alipojipeleka Ikulu Novemba 5, 2009 akatangaza kuitambua serikali yake.
Alisema
matamshi ya Dk Magufuli katika hotuba zake zote, ameweka bayana kila
kitu, amewakanya wanasiasa wachochezi na hatarishi kwa amani, amewaonya
viongozi katika serikali zote huku akikataa uzembe, urasimu, ubadhirifu
wa mali za umma na kusema wote wasiotosha, wajipime iwapo bado wanafaa
au la.
0 comments:
Post a Comment