Jeshi
la Polisi limelazimika kufyatua risasi angani na kutumia mabomu ya
machozi kuwatawanya wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) wanaodhaniwa
kuwa ni wafuasi wa aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof. Lipumba
waliokuwa wakimzuia mwenyekiti wa muda wa CUF, Julius Mtatiro, kuingia
ofisini eneo la Buguruni.
Wafuasi
hao wameeleza kuwa wameamua kumzuia kwani Msajili wa Vyama vya Siasa
ametaka shughuli zozote ndani ya CUF zisiendelee hadi hapo mgogoro wa
uongozi utakapotatuliwa.
Itakumbukwa
hivi karibuni CUF kilimteua Julius Sunday Mtatiro kuwa mwenyekiti wa
muda baada ya mwenyekiti aliyekuwepo, Prof. Lipumba kijiuzulu Agosti
2015.
Julius
Mtatiro leo amefanya mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za
Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam ili kuzungumzia kauli
zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe
Magufuli akiwa visiwani Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment