Thursday, September 1, 2016

MENO YA TEMBO YAKAMATWA MKOANI IRINGA NA ABIRIA 14 WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI

 kamanda wa pilisi mkoa wa iringa Julias Mjengi akiwaonyesha waandishi wa habari vipande nane vya meno ya tembo vilivyokamatwa kwenye gari katika eneo la mbalaziwa katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa

kamanda wa pilisi mkoa wa iringa Julias Mjengi akiwaonyesha waandishi wa habari vipande nane vya meno ya tembo vilivyokamatwa kwenye gari katika eneo la mbalaziwa katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa 

 NA RAYMOND MINJA IRINGA

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa linawashikilia abaria kumi na nne waliokuwa wakisafiri na gari ndogo aina ya haice iliyokamatwa  na meno ya tembo vipande  nane vyenye uzito wa kilogramu 20 vyenye thamani ya sh milioni 66,600.00 walikokuwa wakisafiri kutoka mbeya kwenda Dar esaalam .


Abiria hao wamekutwa wakiingia mikononi mwa jeshi la  polisi baada ya kondakta na dereva wa gari hilo kuchanja mbuga  mara baada ya kugundua polisi wameona nyara hizo za serekali  zinazosakwa usiku na mchana .


Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa  Julias Mjengu alisema kuwa tukio hilo lilitokea agust 31 majira ya saa 18;10 za jioni katika kijiji cha nyololo kata ya nyololo tarafa ya malangali  katika wilaya ya mufindi mkoani Iringa


Mjengi alisema kuwa gari hilo lilikamatwa na askarino E.7998CPL Kaisi aliekuwa akirudi nyumbani kwake akiwa katika eneo hilo la mbaramaziwa alisimamisha gari yenye namba za usajili T377DCX Toyota hiace ikiwa na abiria 14 ndani yake na ilipoikagua aligundua gari  hiyo haina route ya Iringa bali ilikuwa na route ya  mbeya mjini na tunduma .


“Baada ya askari kushuku gari hiyo alimuamuru kundakta kufungua buti la gari ili kuweza kulikagua na alikutana na mabegi mengi huko kwenye buti lakini katika begi moja jeusi alipolifungua alikutana na hayo meno ya tembo vipande nane vilivyokatwa katikati ambapo ni sawa na  tembo wawili waliouwawa


Kamanda Mjengi alisema kuwa mara baada ya askari kuona nyara hizo za serekali dereva wa gari hilo pamoja na kondakta wake walitimua mbio na kuingia msituni huku wakilitelekeza gari hilo pamoja na abiria walimukuwa ndani yake.


Hata hivyo  alisema kuwa jeshi hilo linawashikilia wote walimokuwa ndani ya gari hiyo   kwa mahojiano zaidi ili kuweza kubaini ukweli wa tukio hilo huku msako mkali ukiendelea ili kuweza kuwakamata waliokimbilia porini .

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More