Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga wakionyesha mfano wa sare za wanafunzi walizotoa msaada
Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga wakiwa tayari kukabidhi sare kwa wanafunzi
Hawa ni baadhi ya wanafunzi mia mbili (200) wanaoishi katika mazingira magumu wanatarajiwa kusaidiwa msaada wa pesa kwa ajili ya kununulia sabuni,nauli kila wiki na sare za shule ya msingi.
NA FREDY MGUNDA,Iringa
ZAIDI ya wanafunzi mia mbili
(200) wanaoishi katika mazingira magumu wanatarajiwa kusaidiwa msaada wa pesa
kwa ajili ya kununulia sabuni na nauli kila wiki na wanawake walionda timu
maalum ya kutoa msaada kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Msaada huo unatarajiwa
kutolewa kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kutoka kata nne
zilizoko manispaa ya Iringa ambazo ni Miyomboni, Igumbilo, Kitanzani na Ruaha
na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 3.5
Akizungumza wakati wa kuwakabidhi
msaada wa sare za shule,viatu na soksi wanafunzi hao, katika hafla fupi ya iliyofanyika
katika shule ya msingi ya Igumbulo, Diwani wa
viti maalum CHADEMA Sara Mwajeka
alisema kuwa wameamua kuwasaidia wanafunzi hao kwa lengo la kuwapatia elimu bora
japo kuwa misaada hiyo haiwezi kumaliza shida zao.
Mwajeka aliongeza kuwa wanafunzi
wenye mazingira magumu wanatakiwa kusoma ili taifa lipate wasomi wengi wenye
tija ya kuisaidai nchi yao kuendelea kiuchumi.
“Mimi kama mama napata
uchungu kuona wanafunzi wenye mazingira magumu wanasoma kwa taabu huku wana uwezo
mkubwa darasani,hivyo tunajitaidi na kujikuna pale tunapoweza kuwasaidia
wanafunzi nawaomba watu wenye uwezo kuwasaidia wanafunzi wote wenye mazingira
magumu” alisema Mwajeka.
Kwa upande wake Naibu Meya
wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata aliwapongeza timu ya wanawake wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa kwa kutoa msaada huo ambao ni mkubwa
kwa maisha ya wanafunzi wanaoishi kwenye mazingira magumu.
“Tanzania yetu kuna matajiri
wengi sana lakini wanashindwa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira
magumu lakini wakimama hawa wamejitoa kwa kile walicho nacho kuwasaidia
wanafunzi hao hivyo nami naunga mkono kuendelea kuchangia watoto hawa” alisema
Lyata
Aidha Lyata aliwataka
viongozi wa nchi kuwaangalia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu ili
kufuata na kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo kwani alikuwa anapenda sana
elimu ili wananchi waweze kuongeza ufahamu na kujua mbinu za kujitegemea na sio
kuomba omba kila siku.
“Jamani kusaidia wanafunzi
wenye mazingira magumu hawana idikadi ya vyama,dini wala makabila tunatakiwa
kuwasaidia kutokana na uwezo wetu wa kifedha,mm nimekuwa mwalimu kwa muda mrefu
na nayajua matatizo ya wanafunzi wenye mazingira wanavyosoma kwa taabu ni aibu kwa taifa kama
Tanzania kuwa wanafunzi wanaoteseka kama hawa” alisema Lyata.
Naye Mwalimu mkuu wa shule
ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga aliwashukuru timu ya wanawake wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Naibu Meya, Joseph Lyata kuwa kuwasaidia
wanafunzi wa shule hiyo kwani wamewapunguzia na kuwaondolea aibu iliyokuwa
inawakumba kutokana na umasikini wao.
“Wanafunzi hawa walikuwa
wanavaa sare ambazo zilikuwa zimechanika na ilikuwa aibu kwa wanafunzi wengine lakini
kwa msaada huu mmefanya wajisikie nao ni matajiri na najua sasa watasoma kwa
bidii bila kujiangalia wamekaaje
hongereni sana na karibuni tena kuendelea kuwasaidia wanafunzi hawa” alisema
Asenga.
Misaada hiyo imetolewa na
timu ya wanawake wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) manispaa ya
Iringa kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye mazingira magumu wasome wakiwa na
furaha kwa kuwa nao ni binadamu kama binadamu wengine.
0 comments:
Post a Comment