Na Mwandishi Maalum, New York
Shirika
lisilo la Kiserikali la Speak Up for Afrika limemtunukia tuzo,
Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kutokana na uongozi wake wa kisiasa
na utetezi wake kwa makundi ya jamii yaliyo katika mazingira magumu
hususani wanawake na watoto.
Utoaji
wa Tuzo hiyo ya uongozi wa kisiasa na utetezi , umekwenda sambamba
na hafla ya miaka mitano ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Speak up
Afrika. Hafla hiyo iliyofanyika jana Alhamisi Jijini New York
ilikuwa pia ni sehemu ya kuhamasisha uchangiaji wa shughuli za
Taasisi hiyo.
Mchango
ambao umetambuliwa na Speak Up Afrika, taasisi ambayo imekuwa
ikifanya kazi kwa Karibu na Rais Mstaafu Kikwete, ni katika maeneo ya
upelekaji na usambazaji wa huduma za msingi za afya hususani afya ya
mama na mtoto, udhibiti wa ugonjwa wa malaria kupitia kampeni ya
malaria haikubaliki ,usambazaji wa vyandarua vyenye viatilifu, kampeni
ya lishe bora, na kampeni ya chanjo kwa watoto.
Pamoja
na kutambua juhudi za Rais Mstaafu Kikwete katika kuyasemea
maeneo hayo, Taasisi hiyo kupitia Mkurugenzi wake Mtendaji Bi. Kate
Campana pia imemtambua kama kiongozi ambaye amekuwa mstari wa mbele
wa kulisema Bara la Afrika kila mara alipopata fursa ya kufanya
hivyo wakati akiwa madarakani na hata baada ya kustaafu.
Rais
kikwete ameelezwa katika hafla hiyo iliyowashirikisha wadau wa kada
mbalimbali, kama kiongozi wa kisiasa ambaye amezigusa nyoyo za watu
wengi kujitolea kwaajili ya watu wenye mahitajio ya kupata huduma za
msingi za kijamii ambazo au wameshindwa kuzipata kutokana na kipato
kidogo au haziwafikii kabisa.
Akipokea
Tuzo hiyo, Rais Mstaafu Kikwete , amesema Tuzo hiyo ni ya watoto wote
waafrika ambao ndio waliomfanya asimame mbele ya wageni waalikwa.
“
Ni kwa sababu yenu ndio sababu nimetenga muda wangu baada ya kustaafu
kusukuma mbele agenda ya kuboresha maisha yanu. Ninafanya hivyo
kwasababu makuzi yangu yalikuwa kama ya mtoto yeyote yule wa kiafrika,
nimeyaishi maisha wanayo ishi. Na kwa hiyo ninaelewa fika hamu na kiu
yao ya kuwa na maisha bora na afya njema”. Akasema Kikwete na
kushangiliwa na wageni waalikwa.
Akaongeza
kuwa , mafaniko ambayo ameyapata katika juhudi hizo za kufikisha
huduma za msingi za kijamii kwa makundi yenye mahitaji yametokana na
mambo mawili makubwa moja ni aina ya uongozi alioutumia kusukuma
harakati hizo. Na pili uhamasishaji uliofanyika katika kupiga vita
malaria kupitia Speak Up Afrika na kampeni yao ya malaria
haikubaliki.
“
Nisingeweza kuyafanya niliyoyafanya bila uungugwaji mkono na
ushirikiano wa karibu nilioupata na ninaoupata kutoka taasisi za
kimataifa ikiwamo hii ya Speak Up Afrika. Ndio maana kwa mfano,
tumeweza kupunguza visa vya malaria kwa theluthi mbilli,
tumefanikisha upatikanaji wa chanjo kwa asilimia 96 kwa watoto wote na
kupunguza vifo vitokanavyo na malaria kwa nusu.” Akaeleza Kikwete na
kushangiliwa tena.
Akasema,
anamini katika ushirikiano na wadau mbalimbali kama akina Ray Chambers
kupitia kampeni ya hakuna tena malaria, Taasisi ya Bili na Melinda
Gates na Gavi Vaccination Alliance ambayo anashirikiano nayo kwa
karibu katika kampeni ya chanjo kwa wote.
Rais
Mstaafu amewahakikishia watendaji wa Speak Up Afrika kwamba
ataendelea kufanya kazi nao kwa karibu kutokana kile alichosema
amejionea mwenye kazi nzuri wanayoifana.
Akawasihi
wadau mbalimbali kuichangia taasisi hiyo kwa kile alichosema,
inafanya kazi kubwa ya siyo tu kufikisha huduma za kijamii pale
zinapotakiwa lakini pia imekuwa ni kipaza sauti cha Afrika.
Wengine
waliopewa Tuzo kwa kutambua michango yao kwa jamii ni pamoja na
Professa Awa Marie Coll- Seck, Waziri wa Afya wa Senegal, Bibi Toyin
Saraki, mwanzilishi wa Taasisi ya Wellbeing Afrika ambayo pia
imekuwa ikitoa elimu na misaada kwa wanawake na watoto pamoja na elimu
kwa wakunga na kutambua kazi nzuri, kubwa na ngumu ya kuwahudumia
wanawake wenzao wanapojifungua. Na Bwana Kabirou Mbodje ambaye ni
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Wari.
Taasisi
ya Speak Up Afrika imeanzishwa na wanawake na inaongozwa na
wanawake. Ni taasisi ambayo imejijengea uweo na sifa kubwa ndani ya
kipindi cha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake.
0 comments:
Post a Comment