Thursday, September 8, 2016

SIKU YA KUSOMA DUNIANI: ROOM TO READ WADHAMIRIA KUONDOA UJINGA KWA VITENDO

 Watoto wanafunzi wa Darasa la kwanza kutoka Shule ya msingi ya Zinga wakiwa wanaweza kusoma vitabu wakiwa na miezi sita tuu ya darasani kupitia Programu ya Room to read
 Watoto wa Darasa la kwanza Shule ya Msingi ya Zinga iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani wakiwa wanajifunza matamshi ambapo mpaka sasa wanaelewa vizuri na hizi ni juhudi kubwa zinazofanywa na Shirika la Room to Read.
 Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Zinga Msafiri Tolla akielezea namna walivyoweza kunufaika na Programu ya Room to Read ambapo amelishukuru shirika hilo na  ameeleza mafanikio waliyo yapata kutokana na kujengewa Maktaba na Darasa ikiwa ni pamoja na kuwa imesaidia kupunguza upungufu wa Madarasa, katika Maktaba imeweza kusaidia kiwango cha usomaji kwa wanafunzi na kufanya wanafunzi wengi kupenda kusoma shuleni hapo, na imewawezesha hata wanajamii wanayo izunguka shule kuwa na utaratibu wa kujisomea katika Maktaba hiyo, mwisho alisema kuwa kwa sasa wanafunzi wanaweza kujisomea wenyewe bila matatizo
Afisa Elimu Taaluma Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani Bi. Ester Lumato akielezea umuhimu wa Shirika la Room to Read ambapo katika shule ya Msingi Zinga walianza kufanya nao kazi kuanzia mwaka 2015,alisema miaka ya nyuma iliyopita taaruma ilikuwa chini lakini baada ya kuanza kufanya kazi na Room to Read kiwango hicho cha taaluma kimeongezeka zaidi. Ameongeza kuwa zamani mwanafunzi alikuwa anamaliza darasa la Saba hajui kusoma wala kuandika lakini kwa sasa wanamaliza wakiwa wanajua hayo yote kwa sababu ya shirika hilo kutoa Maktaba na Vitabu vya kutosha, mwisho alitoa wito kwa Mashirika mengine kujitoa kama Room to Read
 Joackim Kawa Meneja wa mradi wa Usomaji na maktaba kutoka Shirika Room to Read akielezea miradi ambayo wanaendesha ikiwa katika shule za Msingi wanatekeleza Mradi wa Maktaba na Kusoma ambapo kuna walimu maalum  katika shule 62 za Bagamoyo wanaandaliwa kuhakikisha wanafunzi wanaweza kusoma na na kuandika vizuri,ambapo mradi huu umetekelezwa Mkoani Morogoro pia aliongeza kuwa wanampango wa kupanua wigo zaidi wa miradi yao katika maeneo mengine nchini Tanzania
 Hii ni maktaba ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read ambapo kuna vitabu vya aina mbalimbali vya masomo kuanzia Darasa la Kwanza mpaka la Saba 
Wanafunzi wakiwa wametulia wanasoma vitabu katika maktaba yao ambapo kila mmoja anaamua asome kwa namna gani  
Wanafunzi wa Darasa la kwanza wakiwa wanaendelea kusoma
Hapa kila mmoja anaelewa anacho kisoma hii ni kutokana na kuwa na walimu ambao wamewezeshwa na Shirika la Room to Read ambapo wamekuwa wanaweza kusoma na kuandika vizuri 
Wanafunzi wa Darasa la kwanza Shule ya ya Msingi Zinga wakiwa wanafurahia kupata Vitabu kutoka Shirika la Room to Read
 Wanafunzi wakiwa wanachambua vitabu kwa ajili ya kujisomea katika maktaba ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read.
 Hii ni Maktaba ya Shule ya Msingi ya Kiromo ambayo imewezeshwa na Shirika la Room to Read
 Mwalimu Naomi anangisye ambaye anafundisha darasa la kwanza Shule ya Msingi Kiromo alieleza kuwa kabla ya Shirika la Room to Read hawajaanza kufanya kazi katika shule hiyo kulikuwa na shida ya ufundishaji katika madarasa yao,lakini baada ya Shirika hilo kuanza kazi katika shule hiyo waliwapa mafunzo ambayo yamewasaidia kwa kiasi kikubwa katika ufundishaji na kwa sasa wanafunzi wengi wanajiweza katika kusoma, aliwaomba Shirika la Room to waendelee hivyo ili kuja kutokomeza kabisa tatizo la Ujinga
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Kiromo Bi. Flora Mlowe  alisema kuwa mradi wa Room to Read umeinufaisha sana shule yake kwanza wameweza kupata chumba cha kusomea amacho kimewasaidia sana wanafunzi tofauti na ilivyokuwa mwanzoni, aliongeza kuwa mradi huo umewafanya wanafunzi waweze kuongeza juhudi za kujisomea, wanasoma kwa burudani na pia wanapata maarifa mbalimbali kupitia vitabu hivyo, hiyo imesaidia kuondoa kundi kubwa la wanafunzi ambao hawajui kusoma alimaliza kwa kusema kuwa kuwepo kwa Maktaba hiyo kutaongeza zaidi ufauru katika shule yake.
 Furaha Tonya Social Mobilizer wa Shirika la Room to Read Tanzania akiwa katika Shule ya Sekondari Matibwa iliyopo Bagomoyo akielezea mradi wa Elimu kwa mtoto wa Kike Tanzania unaoendeshwa na Shirika la Room to Read ambapo moja ya mambo wanayo fundisha ni Life Skills ambapo lengo kubwa ni kuwataka watoto waweze kujitambua.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Matibwa Ally Kilasama alisema kwamba mradi huo umeweza kuwasaidia watoto wengi zaidi wa kike kuwepo katika shule hiyo, katika mradi wa life skills alisema kuwa kwa sasa watoto wa kike  wameweze kujitambua zaidi na watoto wa kike wanafanya vizuri zaidi kulipo wale wa kiume, pia kupitia mradi huo kutoka Room to Read wameweza kupata vifaa ya Sayansi na vitabu vya kutosha kwa wanafunzi na kwa sasa wanakarabati madarasa manne hii ikiwa ni juhudi za kutokomeza ujinga.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kingani wakiwa darasani wanamsikiliza mwalimu
 Kutokana na wanafunzi wakike kuelewa Elimu ya Life Skill wameweza kuwaburuza wanafunzi wa kiume katika ufauru darasani ambapo katika Kidato cha tatu Mchepuo wa Sayansi shule ya Sekondari Kingani Mwanafunzi mmoja tu wa kiume  ndiye ameweza kuingia katika kumi Bora ambapo hapa anaelezea jinsi kulivyo na changamoto ya ushindani katika darasa hilo na kukili kuwa watoto wakike wanaweza sana 
 Rose Jeremiah Ngalya Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu Mchepuo wa Sayansi aliye ongoza na kushika nafasi ya kwanza akieleza namna ya Shirika la Room to Read lilivyo wasaidia katika kuhakikisha wanapata Elimu Bora.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More