Bilionea
namba moja barani Afrika, Aliko Dangote amekanusha uvumi unaosambaa
kwenye mitandao ya kijamii kuwa amefariki dunia akiwa nchini Ujerumani.
Taarifa
hizo zinaeleza kuwa bilionea huyo amefariki akiwa nchini Ujerumani
baada ya kuugua kwa muda mfupi. Aidha, taarifa hizo zinaeleza kuwa
familia ya bilionea huyo imethibitisha kifo cha ndugu yao huyo na kusema
kuwa ni pigo kubwa kwa Afrika.
Kupitia
ukurasa wake wa Twitter, Dangote ameandika hivi “I am hale, hearty and
alive. Please disregard malicious report saying otherwise. Thank you.” ,
akimaanisha kuwa yeye ni mzima wa afya na kuwataka watu kupuuzia
taarifa zinazoeleza kivingine.”
Akimaanisha “Mimi ni mzima na buheri wa afya. Tafadhali puuzeni taarifa zote zinazosema vinginevyo. Asanteni.”
Aliko
Dangote ni raia wa Nigeria, ndiye mwenye utajiri mkubwa zaidi barani
Afrika. Dangote anamiliki kampuni kubwa ya Dangote Group inayofanya kazi
katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwa ni pamoja na Nigeria, Benin,
Ethiopia, Senegal, Cameroon, Ghana, Afrika Kusini, Togo, Tanzania na
Zambia.
Muda
mfupi baada ya kuzuka kwa taarifa hizo, Aliko Dangote alikanusha
taarifa hizo kupitia mtandao wa Twitter kwa kupost kuwa yuko Afrika
kusini na yuko salama kabisa.
0 comments:
Post a Comment