Tuesday, September 27, 2016

MAONYESHO YA FILAMU ZA BEIJING 2016 CHACHU KWA UKUAJI WA SANAA NCHINI


 Washindi wa kwanza hadi wa tatu wa mashindano ya sauti waliopatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China wakionesha tuzo baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Washiriki 10 walishinda mashindano hayo. Kutoka kushoto ni Hilda Malecela, Safiya Ahmed na Sadiq Kututwa.


Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akisalimiana na mmoja wa washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Anastazia Wambura akizungumza na washindi hao.

 Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,. Anastazia Wambura akiwasisitizia jambo mshindi wa kwanza hadi wa tatu baada ya kuwakabidhi tuzo zao.
 Washindi 10 wa mashindano ya vipaji vya sauti, Abraham Richard, ambao watakakwenda kufanya kazi makao makuu ya StarTimes jijini Beijing, China wakiwa katika picha ya pamoja na kutoka (kushoto) Muwakilishi wa Mamlaka ya Halmashauri ya Beijing, Yang Peili,  Meneja Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa, Dk. Ayoub Riyoba, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura, Muwakilishi wa Ubalozi wa China nchini,  Guo HaoDong, Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,  Guo ZiQi na Kansela wa Utamaduni katika Ubalozi wa China nchini Tanzania, Gao Wei wakati wa hafla fupi ya Maonyesho ya Matangazo ya Tamthiliya za Runinga na Filamu za Beijing 2016.
 Washindi hao 10 wakifurahia baada ya kukabidhiwa  tuzo.

Na Dotto Mwaibale

STARTIMES  imefanya Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na Filamu za Beijing ya mwaka 2016 kwa mara ya pili jijini Dar es Salaam kwa lengo lakuendelea kukuza ushirikiano wa iutamaduni baina ya China na Tanzania.

Akizungumza wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam leo asubuhi, mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema kuwa kwa muda mrefu serikali ya China na Tanzania zimekuwa na 
mahusiano mazuri katika Nyanja za kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

“Mahusiano mazuri ya kiutamaduni ndiyo yaliyopelekea serikali hizi mbili kuendelea kushirikiana na kuwa marafiki mpaka hivi leo. Uhusiano huo si tu unatunufaisha katika masuala ya kiuchumi bali pia kijamii. 

Kupitia kazi za sanaa kam vile tamthiliya za michezo ya kuigiza na filamu watu huweza kujua na kujifunza tamaduni za kila upande. 

Nawapongeza StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China nchini Tanzania kwa kutuletea maonyesho haya ambayo nina hakika yatakuwa na manufaa makubwa kwa tasnia yetu.” Alisema . Wambura

“Pia ningependa kuwapongeza StarTimes kwa juhudi zao za dhati katika kukuza utamaduni wetu kuipa nafasi lugha ya Kiswahili kuwa mojawapo inayotumika kutafsiri filamu na tamthiliya hizi za 
michezo ya kuigiza. Nimesikia mlifanya shindano la vipaji vya sauti ambapo watanzania kumi walipatikana na watakwenda kufanya kazi katika makao yenu makuu yaliyopo Beijing. 

Hii ni hatua nzuri na jambo la kuigwa kwa kukipa Kiswahili nafasi kubwa. Ninegependa kumalizia kwa kutoa wito kwa washindi waliopatikana kwenda huko China kutuwakilisha vema kama mabalozi wetu na kukifanya Kiswahili kiendelee kutambulika zaidi.” alisema Wambura

Akielezea umuhimu wa maonyesho hayo Makamu wa Rais wa Makampuni ya StarTimes,. Guo ZiQi amebainisha kuwa kihistoria China imedumisha kwa dhati urafiki na mataifa ya Afrika na kushirikisha tamaduni ndio njia madhubuti itakayoenzi mahusiano hayo.

‘’Utofauti ndio unaofanya dunia pawe mahala pazuri pa kuishi na China na Tanzania kwa muda mrefu zimedumisha utamaduni wao unaovutia zaidi. Katika kilele cha mkutano wa jukwaa la ushirikiano baina ya China na Afrika uliofanyika mwaka 2015, Rais wa Jamhuri ya watu wa China, 

 Xi Jinping alionesha nia ya kujizatiti katika kudumisha mahusiano mazuri ya kiutamaduni, kuimarish mafunzo baina ya China na Afrika ili kusonga mbele kwa pamoja na vilevile kuhakikisha mustakabali wa ukuaji wa urafiki baina ya China na Afrika.’’Alisema  ZiQi

‘’Kwa kuendelea kukua kwa mahusiano ya maingiliano ya kiutamaduni baina ya watu wa China na Waafrika, michezo ya kuigiza ya runinga na filamu za Kichina imezidi kujizolea umaarufu na kuwa kichocheo muhimu katika kujenga mahusiano baina ya pande hizo mbili. Kwa hivi sasa Beijing inaongoza China katika uzalishaji wa michezo ya kuigiza ya runinga na filamu. 

Mpaka hivi sasa ina taasisi takribani 3,400 zilizojikita katika uzalishaji wa filamu na vipindi vya uninga na uendeshaji, vikiwa tayari vimekwishazalisha zaidi ya mfululizo wa vipindi vya runinga 3,000 na karibuni filamu 300 kwa mwaka.’’ alisema ZiQi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Teknolojia na Ufundi ambaye alizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Wang Xiabo alisema kuwa,‘’mnamo mwaka 2014, Halmashauri ya Mamlaka ya Uandishi wa Habari, Uchapishaji, Redio, Filamu na Runinga ya Beijing ilishirikiana na StarTimes kuzindua msimu wa Maonyesho ya Michezo ya Kuigiza ya Runinga na 
Filamu za Beijing katika nchi za Kiafrika. Lengo kubwa lilikuwa ni kuleta simulizi nyingi za Kichina barani Afrika na kukuza uhusiano katika tasnia za filamu na runinga baina ya pande mbili.’’


‘’Maonyesho haya yamefanyika kwa mafanikio makubwa kwa miaka ya 2014 na 2015 mfululizo. Filamu maarufu za Kichina na mfululizo wa michezo ya kuigiza ya runinga  ambayo imeingizwa sauti kwa lugha ya Kiingereza, Kifaransa na lugha nyinginezo tano za Kiafrika zilionyeshwa na StarTimes kwa miaka hiyo iliyopita,’’ alisema Wang Xiabo kuwa,‘’Katika kipindi hiko tamthiliya kama zilipata mapokezi makubwa sana kutoka kwa hadhira ya barani Afrika.


Meneja Mkuu wa Shirika la Utangazaji waTaifa (TBC),  Ayoub Riyoba, ambao ni washirika wa kampuni ya StarTimes katika urushaji wa matangazo ya dijitali nchini Tanzania amebainisha umuhimu wa filamu hizo hususani katika ukuzaji wa tamaduni baina ya nchi hizo mbili.

‘’Tanzania na China zina historia ndefu ya mahusiano tangu enzi hizo za waasisi wa mataifa haya. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Sisi kama chombo cha habari cha taifa tumekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa tunasaidia jitihada za 
serikali kukuza na kuutangaza utamaduni wetu hususani lugha ya Kiswahili. Kwa takribani miaka miwili iliyopita TBC imekuwa ikionyesha tamthiliya za Kichina zilizoingiziwa sauti kwa lugha ya Kiswahili. 

Kwa kufanya hivyo hivyo tamthiliya hizo zimeonyesha kupokewa vizuri na kupendwa sana na watanzania kwani wamekuwa wakielewa kinachoonekana.’’ alisema Riyoba

‘’Mbali na kukuza lugha yetu ya Kiswahili nchini na nje yanchi, hii pia ni fursa kwa tasnia yetu ya filamu kujifunza kutoka kwa wenzetu ambao wamepiga hatua zaidi. Tasnia yetu bado ni change na inahitaji mengi ya kujifunza ili kusonga mbele na kufikia pale walipo wenzetu na kuwa inazalisha kazi nyingi zaidi za sanaa. 

Ningependa kuchukua fursa hii kuipongeza na kuishukuru serikali ya China kwa jitihada zao wanazozionyesha katika kukuza filamu na lugha yetu ya Kiswahili. Na ningependa kuwaahidi kutokana na ushirikiano huu watazamaji wa TBC wataendelea kupata burudani ya tamthiliya 

na filamu nzuri zaidi ya zilizopita.’’  alisema Meneja Mkuuwa TBC katika maonyesho hayo Ubalozi wa China nchini Tanzania pia ulikabidhi mfano wa hati za makubaliano ya kwenda kufanya kazi 
jijini Beijing kwa washindi 10 waliopatikana katika shindano la vipaji vya sauti lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Dar es Salaam.

Washindi hao 10 waliopatikana ni; Hilda Malecela(DSM), Safiya Ahmed(ZNZ), Saiq Kututwa(ZNZ), Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala Abdul(DSM), Rukia Hamdan(ZNZ), Richard Rusasa (DSM), Happiness Stanslaus - Nyamayao (DSM), Jamila Hassan(DSM) na Abraham Richard (DSM).

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More