mwanamuziki wa nyimbo za injili Mess Jakobo Chengula
akionyesha cheti ya hehima cha balozi wa amani alichozwadawa na serekali
ya ya Kongo
Serekali ya Jamuhuri ya Demokrasia ya Kongo imemtunuku cheti cha
heshima ya kipekee cha {Balozi wa Amani }
mwanamuzi wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Mess Jakobo Chengula kwa kazi
nzuri anayoifanya ya kuhubiri amani na upendo kupitia nyimbo zake .
Mess Jakobo Chengula ambaye kwa
sasa anatamba na wimbo wa moyo wangu hauna woga aliomshirikisha mwanadada
Upendo Nkone ni mwanamuziki pekee kutoka Tanzania aliyotunikiwa cheti hicho cha
heshima cha balozi wa Amani ulipokwenda
kufanya huduma ya uimbaji katika nchi ya Kongo
Akizungumza na mtanzania Chengula
alisema kuwa ni heshima ya kipekee aliyoipata yeye na taifa lake la Tanzania kwa watu wa mataifa mengine kuona mchango wa wuziki
wa injili katika kuhubiria Amani ya dunia
na afrika kwa kiujumla .
Chengula alisema kuwa cheti
alichopewa ni cheti cha heshima ya ulinzi wa Amani kutokana ujumbe mzuri ulioko
katika nyimbo zake na matendo mema afanyao
katika huduma yake hivyo ni farahi ya kipeke kwa nchi ya Tanzania kuonekana ni
nchi inayoendeshwa kwa misingi ya Demokrasia na haki jambo lililopelekea hata
mataifa mengine kuona haja ya kuwapa cheti wanamuziki wanaohubiri Amani kutoka tanzania
“Unajuaa pale tulienda katika
huduma ya kuhubiri neno la Mungu na uimbaji na tulikutana watu kutoka mataifa mbalimbali na
mimi peke yangu ndiye niliyotokea Tanzania na pale kulikuwa na viongozi
mbalimbali na waimbaji wengi tena wakubwa
kutoka mataifa makubwa lakini hawakupewa
cheti cha balozi wa Amani lakini mimi
nilipewa asee hii ni heshima ya pekee ambayo Tanzania imepata kupitia mimi kule
nchini Kongo “”.
“Kongo wamenionyesha kitu cha ajabu
sana unaju nchi za wenzetu wanamuziki wanaheshimika sana unajua mimi nimefanya
muziki muda mrefu hapa nchini alibamu yangu ya kwanza ni ile ya Mungu wangu
habadiliki lakini sijawahi kupata mapokezi makubwa na ya kipeke kama yele niliyopata
kule kongo hapa kwetu kuna heshima Fulani lakini kwa kuwa tumezoeya na
tunaonana kila mara basi kunakuzoeyana lakini Mungu ni mwema tutabadilika tu na
kuthamini cha kwetu lakini kongo ohoo
wametisha maze”
Hata hivyo Mess alisema kuwa
anatarajia kuzindua albamu yake mpya ya moyo wangu hauna woga
inayosambazwa na Msama promotion uzinduzi utakaofanyika jijini Dar eslaam September 20 mwaka huu huku akiwataka wapenzi
na mashabiki wa muziki wa injili kujitokeza kwawingi kwa ajili ya kumsapoti
katika huduma yake
0 comments:
Post a Comment