Tuesday, September 27, 2016

LHRC WASHEREHEKEA MIAKA 21 NA WATOTO WANAOISHI MAKAO YA TAIFA YA WATOTO WENYE SHIDA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM

Wafanyakazi wa LHRC wakijumuika na watoto wanaolelewa katika Makao ya taifa ya watoto wenye shida Kurasini jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 21 tangu kuanzishwa kwake.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk. Helen Kijo-Bisimba (katikati) akiwasaidia watoto kukata keki kusheherekea miaka 21 ya LHRC.
Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.


Na Dotto Mwaibale

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  kimeiomba serikali kupitia wizara ya Afya ,Jamii Jinsia ,Wazee na Watoto, pamoja na na Wizara ya Katiiba na Sheria ,kufanya marekebisho yaSsheria ya Mtoto  nakutilia mkazo malezi bora ya watoto ikiwemo kuweka kipengele kitakacho toa  adhabu kali  kwa familia itakayo shindwa kutoa malezibora kwa watoto au kutelekeza familia.

Akizungumza katika maadhimisho ya  miaka 21 ya kituo cha sheria na haki za binadamu, yaliyofanyika katika Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida kilichopo Kurasini, Temeke Jijini Dar es salaam,  Mkurugenzi Mtendaji wa  kituo hicho Dk. Helen Kijo-Bisimba alisema kuboreshwa kwa sheria hizo kutasaidia kupunguza wimbi la watoto wasio na makao maalumu  wanao zagaa kuomba omba mitaani, na ameitaka jamii  kushiriki katika kutatua tatizo la watoto wa mitaani linalozidi kushika hatamu kila siku.


Ofisa Mfawidhi wa kituo  hicho,  Beatrice Laurence  ame kishukuru kituo cha sheria na haki za Nina damu kwakuona umuhimu wa kutoka misaada katika kuwa saidia watoto wanao lelewa  hapo  nakuwataka watanzania wengine  badala ya kuelekeza nguvu zao  pekee kwa wathirika wa tetemeko huko Kagera  kuwa kumbuka na  watoto yatima kwani nao  wanayo kahitaji ya kibinadamu.


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilianzishwa Septemba 26, 1995 kwa lengo la kufanya utetezi kwa watu wenye uhitaji sambamba na kulinda haki za binadamu nchini.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More