Kituo
cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimefungua milango ya uwekezaji wa nchi
mbalimbali kuja kuwekeza Nchini hasa makao makuu ya Nchi, Dodoma.
Hayo
yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa (TIC), Clifford Tandari juu ya fursa
za uwekezaji zilizopo Mkoani Dodoma, wakati wa Mkutano Mkuu wa
Uwekezaji wa Dunia kanda ya Afrika uliofanyika Mjini Kigali nchini
Rwanda hivi karibuni.
Mkutano huo uliandaliwa na COMESA kwa kushirikiana na Serikali ya Rwanda.
Rais
Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, wakipatiwa
maelezo na Mtendaji Mkuu wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford
Tandari, juu ya fursa za uwekezaji zilizopo Mkoani Dodoma, wakati wa
Mkutano Mkuu wa Uwekezaji wa Dunia kanda ya Afrika uliofanyika Mjini
Kigali nchini Rwanda hivi karibuni.
Rais
Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, wakimsikiliza
kwa makini Mtendaji Mkuu wa Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Clifford
Tandari, alipokuwa akiwaelezea juu ya fursa mbalimbali za uwekezaji
zilizopo Mkoani Dodoma, wakati wa Mkutano Mkuu wa Uwekezaji wa Dunia
kanda ya Afrika uliofanyika Mjini Kigali nchini Rwanda hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment