Monday, February 29, 2016

DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA KWA DUKA LA DAWA LA SHINE PHARMACY LA TEMEKE

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa kwa Duka la dawa za binadamu la Shine Care Pharmacy lililopo Temeke, baada ya kubainika kuendeshwa kinyume cha sharia ikiwemo kutokuwa na kibali cha uendeshaji na mfamasia husika.

Jeshi la Polisi Zanzibar Latoa Ufafanuzi Kuhusu Madai ya CCM Kutaka Maalim Seif Akamatwe

Jeshi la Polisi Zanzibar limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa jeshi hilo linapanga kumkamata Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Kikwete: Nitaachia Uenyekiti wa CCM, Lakini Sitaacha Vikao vya Ndani CCM

Moja kati ya hoja zinazogonga vichwa vya baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mabadiliko ya Uenyekiti wa Chama hicho ambayo yatamuwezesha mzee wa Kutumbua Majipu, Rais John Magufuli kuanzisha operesheni hiyo ndani ya chama hicho.

Mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya yateketea kwa moto

Askari wa Kikosi cha Zimamoto Jijini Mbeya, akiendelea na jitihada za kuuzima moto unaoendelea kuwaka na kuteketeza Mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga jijini humo, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa, na jitihada za kuuzima zinaendelea.

Mashindano ya Tigo Kili Half Marathon yafana mjini Moshi

Maelfu ya wakazi wa Moshi na wanariadha mbalimbali wakifuatilia  mashindano ya Tigo Kili Half Marathon  katika mashindano hayo yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya chuo cha Ushirika Mjini Moshi  

HULE 18 DAR KUNUFAIKA NA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KUTOKA KWA CFAO MOTORS GROUP NA ALLIANCE AUTOS

IMG_4204
Meneja wa Volkswagen nchini, Bi. Tharaia Ahmed (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mafunzo ya elimu ya usalama barabarani ambayo wanataraji kufanya katika shule 18 zilizo katika Manispaa ya Ilala.Mkurugenzi Mtendaji wa CFAO Motors Group, Eric Potin, (katikati) na Mwanzilishi wa mashindano ya mbio za magari ya Go4school, Henning Nathow.

DK.KIGWANGALLA AHIMIZA JAMII KUWA NA UTAMADUNI WA KUPIMA AFYA ZAO MARA MWA MARA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amehimiza Jamii kuwa na utaratibu wa kupima afya mara kwa mara katika hali ya kubaini matatizo yanayowakabili ilikuchukua hatua ikiwemo kupata tiba mapema

Sunday, February 28, 2016

Tafrija ya mchapalo wa uzinduzi wa intaneti ya kasi zaidi ya Tigo 4G Mkoani Kilimanjaro yafana

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa  intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.

NAIBU WAZIRI WA AFYA. DK KIGWANGALLA AKUTANA NA WATAALAM WA MPANGO WA BRN WA WIZARA YAKE

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema leo Februari 27.2016 amekutana katika kikao maalum na Wataalam wa Wizara hiyo ambao wapo katika timu inayoshughulikia Mpango wa Matokeo makubwa sasa (BRN) katika kufanikisha namna ya utoaji huduma bora na ufanisi katika mipango mbalimbali ya kufikia malengo ambayo Serikali ya Tanzania ilianzisha mpangp huo.

Saturday, February 27, 2016

Vurugu Kubwa Zaibuka Wakati wa Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam

VURUGU kubwa zimetokea wakati wa Uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya uchaguzi huo kuhairishwa  tena kwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kuanza kupambana na Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda  UKAWA.

Wafanyabiashara ya Sukari Wamchokonoa Rais Magufuli

SASA ni wazi kwamba wafanyabiashara wa sukari nchini wameamua kuanzisha vita na Rais John Magufuli, kwa kuamua kuficha bidhaa hiyo na hivyo kuadimika katika soko na kupanda bei.

CCM MANISPAA YA IRINGA KUFANYA KONGAMANO LA MIAKA 39 YA CHAMA HICHO KESHO.

 
 KATIBU WA WILAYA YA IRINGA MJINI ELISHA MWAMPASHI

CUF Kuandamana Kupinga Marudio Ya Uchaguzi Zanzibar

CHAMA cha Wananchi (CUF) Bukoba kimejiandaa kufanya maandamano ya amani keshokutwa, kwa ajili ya kupinga kufanyika upya uchaguzi wa Zanzibar unaotarajiwa kuwa Machi mwaka huu.

Majambazi Dar es Salaam Yavamia Benki Ya Access

Majambazi  ambao  idadi  yao  haikufahamika  wakiwa  na  mabomu  na  bunduki  za  kisasa  jana  walivamia  Benki  ya  Access  tawi  la Mbagala  ambako  walipora  viroba vya   fedha, kuua  mlinzi  na  baadae wanne  kati  yao  waliuawa  na  jeshi  la  polisi.

ACTIONAID NA NORAD WAZINDUA MRADI WA KUSAIDIA UBORESHWAJI ELIMU NCHINI

IMG_3912
Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Kimataifa la ActionAid nchini, Dkt. Azaveli Lwaitama akitoa neno la ufunguzi wakati wa warsha ya uzinduzi wa mradi wa kuimarisha elimu kupitia vyanzo vya ndani vya mapato (Promoting Quality Education Through Progressive Domestic Resource Mobilization).

Friday, February 26, 2016

Cosato Chumi akutana na changamoto nyingi wakati wa ziara yake kwenye Taasisi za Umma na Binafsi



Mkurugenzi mkuu wa Green Resources ambao ni kampuni tanzu ya sao hill industry akifafanua jambo kwa cosato chumi mbunge wa mafinga mjini wa pili kulia, Denis kutemile anayefuatia na Hezron Vuhahula ambaye ni katibu wa mbunge

Thursday, February 25, 2016

Mpango wa Push for Change kuwasadia Wakulima katika upatikanaji wa habari za masoko na mitaji

Kongamano la siku tatu juu ya sera ya kilimo linalotarajia kufikia tamati leo Februari 25.2016 huku likiwa limeshirikisha wadau wa kilimo Zaidi ya 150, kutoka ndani ya nje ya Tanzania wametoa maoni yao mbalimbali namna ya kuboresha kilimo hapa nchini ilikufikia maendeleo makubwa.

BLOGU YA WANANCHI YATIMIZA MIAKA MITATU SHEREHE KUFANYIKA KESHO HOTELI YA HYATT REGENCY KEMPISKY JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkuu wa Blogu ya Wananchi, William Malecela 'Le Mutuz' , akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

MH:WILIAM LUKUVI ATOA MSAADA WA PESA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO IDODI

Mbunge  wa  jimbo la Isimani Bw  Wiliam Lukuvi ambae ni  waziri wa Ardhi ,nyumba na maendeleo ya makazi (kulia) akimpa maelekezo mwenyekiti wa  kijiji cha Mapogolo baada ya kumkabidhi fedha  kiasi cha Tsh milioni 2 za  kulipa fidia  ya ardhi kwa  wananchi  watakaohamishiwa makazi mapya  kutoka  kitongoji  cha Kitanewa Idodi ambao  nyumba   zao zilisombwa na mafuriko

Mwanafunzi Wa Kidato Cha Tatu Ajinyonga


Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Nyanungu Tarafa ya Ingwe wilayani Tarime mkoani Mara, Charles Chacha (19), amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya katani.

STATEMENT BY HEAD OF UN MISSION IN TANZANIA ON THE OCCASION OF THE 50TH ANNIVERSARY OF UNDP

Alvaro Rodriguez
UN Resident Coordinator in Tanzania and UNDP Resident Representative, Mr. Alvaro Rodriguez.
Today marks the 50th Anniversary of the United Nations Development Programme (UNDP). Founded in 1966, UNDP now works in some 170 countries and territories to help eradicate poverty and reduce inequalities and exclusion.

MKALI WA NDONDI THOMAS MASHALI KUTAFUTIWA MBABE PASAKA

 Bondia Salum Nassoro akipasha na kocha wake, Maneno Abdallah katika gym yao iliyopo Mazense Midizini.

Donald Trump Azidi Kupeta Mchujo wa Kugombea Kiti Cha Urais Marekani

Mgombea  urais wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda katika Jimbo la Nevada nchini Marekani, na kuzidi kuimarisha uongozi wake katika mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho.

Waziri Mkuu Asubiriwa Kwa Mabango Kiteto

Wananchi  wilayani Kiteto  mkoani  Manyara  wamejiandaa  kumpokea  kwa  mabango  Waziri  Mkuu  Kassim  Majaliwa  ili  kutoa  ujumbe  wa  kuwakataa  baadhi  ya  viongozi  wa wilaya  kutokana  na   kukithiri  kwa  migogoro  ya  ardhi.

Steven Wasira Amkunja Shati Mwandishi Baada Ya Kesi Yake Kupinga Ushindi wa Ester Bulaya

Mwanasiasa mkongwe nchini, Steven Wasira jana alimvamia mpigapicha wa gazeti la Mwananchi aliyekuwa akichukua picha zake wakati akitoka mahakamani, lakini akashindwa kutimiza azima yake ya kufuta picha.

Mafanikio ya kipindi cha Radio cha Walinde Watoto katika kupunguza ukatili kwa watoto

Mratibu wa kipindi cha walinde watoto Neema Kimaro akiongea na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya kipindi hicho pembeni yake ni  Mwandaaji wa kipindi cha Walinde Watoto Kimela Billa katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika studio za True Vision  ambao ndio waandaaji wa kipindi hicho chini ya udhamini wa  UNICEF na uratibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ushirikiano ofisi hizo zipo  Mikocheni, Jijini Dar Es s salaam"

Wednesday, February 24, 2016

Kikwete Kuwatumbua MAJIPU Wanachama Wasaliti wa CCM

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Jakaya Kikwete amesema kuwa chama chake kitawachambua na kuwaadhibu wote ambao walikisaliti katika Uchaguzi Mkuu uliopita, kuanzia ngazi za matawi, kata, wilaya, mkoa hadi Taifa.

MWAKALEBELA AKANUSHA KUFUTWA KWA KESI DHIDI YA MCHUNGAJI MSIGWA

Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wake ubunge jimbo la Iringa Mjini, Frederick Mwakalebela iko pale pale, kikipinga taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii jana na kuchapwa katika baadhi ya magazeti leo kwamba kesi hiyo imefutwa.

Nape aagiza mkataba wa StarTimes na TBC Upitiwe Upya

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameitaka Bodi mpya ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia upya mkataba wa StarTimes na shirika hilo.

Jengo la posta Dodoma lateketea kwa moto

JENGO Posta lililopo katika eneo la sabasaba katika Manispaa ya Dodoma  jana limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa

Ezekiel Maige Atajwa Ufisadi Ngorongoro

Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii katika serikali ya awamu ya nne, Ezekiel Maige, jana alitajwa katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bernard Murunya  ambaye ameshitakiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi.

WANAHABARI, WATAFITI KUTOKA COSTECH WAZURU KABURI LA BABA WA TAIFA BUTIAMA MKOANI MARA

Wanahabari na Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), waliokuwa katika ziara ya kuzungumza na wakulima wa mkoa wa Mwanza kuhusu changamoto za kulimo zinazo wakabili pamoja na matumizi ya bioteknolojia katika kilimo wakiwa mbele ya kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere walipozuru kaburi hilo hivi karibuni Kijiji cha Mwitongo Butiama mkoani Mara.

Tuesday, February 23, 2016

WAKULIMA WILAYANI RORYA MKOANI MARA WAPATIWA MAFUNZO YA KUPATA HUDUMA ZA UGANI KWA NJIA YA SIMU

Mtafiti Kiongozi Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk.Nicholaus Nyange (katikati), akizungumza na wakulima wa Wilaya ya Rorya Mkoani Mara katika mafunzo ya siku moja kwa wakulima hao ya kutumia simu kupashana habari za kilimo na kujua changamoto zinazo wakabili. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia za Kilimo Afrika (OFAB), Daniel Otunge na kushoto ni Mtafiti Mkuu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Dk.Emmarold Mneney.

Rais Mugabe Atimiza miaka 92

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametimiza umri wa miaka 92 huku chama chake kikisema atawania tena urais 2018.

Lipumba Amtaka Rais Magufuli Atangaze Mshahara Na Marupurupu Yake

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Rais John Magufuli atangaze mshahara na marupurupu yake, kwa kuwa amejivisha joho la kuwa Rais wa wanyonge.

Meneja wa Shirika la Posta Tanzania Afikishwa Mahakamani Kwa Matumizi Mabaya Ya Ofisi

Meneja wa Shirika la Posta Tanzania (TPC) Mkoa wa Dar es Salaam, Lawrence Mwalumwelo na wenzake wawili wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka.

Waziri Mkuu Majaliwa apokea Misaada Ya Maafa Ya Sh. Milioni 86/-

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea misaada mbalimbali yenye thamani ya sh. milioni 85.88/- kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko kwenye vijiji vya kata ya Mlenge, tarafa ya Pawaga,  wilaya ya Iringa vijijini mkoa wa Iringa. 

Monday, February 22, 2016

TAZAMA DARAJA LA WATEMBEA KWA MIGUU LA FURAHISHA JIJINI MWANZA

Baada ya Serikali kukamilisha Ujenzi wa Darala la juu la Watembea kwa Miguu katika Eneo la Mabatini Jijini Mwanza na kupunguza wingi wa ajali pamoja na msongamano wa magari katika eneo hilo, Sasa juhudi zimehamia katika eneo la Furahisha Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambapo pia linajengwa Daraja la juu la Watembea kwa Miguu ili kukabiliana na foleni katika eneo hilo ambalo limejengwa pia Kitega Uchumi cha Kisasa cha Rock City Mall ambayo ni Mall (Soko) Kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

BAJETI YAPITISHWA MUFINDI , STORI SAHIHI TADHALI


Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limepitisha  bajeti ya zaidi ya Sh. 67,613,232,516 Katika kikao maalum cha baraza la Madiwani kwa mwaka  2016/2017  ikiwa ni makisio ya mwaka mpya  wa fedha utakaoanza mwezi wa 07 mwaka huu. 

Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Februari 22

Jecha Adai Maalim Seif Ni Mgombea Halali Na ZEC Haitambui Kujitoa Kwake

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, ameibuka tena na kutangaza kukamilika kwa matayarisho ya uchaguzi wa marejeo Machi 20, mwaka huu huku akikataa kutoa majina ya wagombea.

“WATANZANIA WAZINGATIE SHERIA ZA MTANDAO, KIFUNGO NI MIAKA 30 AU ZAIDI” – KITWANGA


Charles Kitwanga 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles Kitwanga (pichani) amewataka Watanzania kuzingatia sheria za mtandao ambazo zilitungwa mwaka jana kufuatia kuonekana kuwepo kwa baadhi ya watumiaji ambao wamekuwa hawafati sheria.

MUNGY AWATAKA WATANZANIA KUZINGATIA MASHARTI NA KANUNI ZA MITANDAO (AUDIO + VIDEO)

Mungy
Mkuu wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy.
Ili kuhakikisha kunapungua kwa makosa ya uvunjifu wa sheria ya mtandao, Mkuu wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), Innocent Mungy amewataka watumiaji wa mitandao kuzingatia kanuni na masharti ya mitandao.

Sunday, February 21, 2016

Magazeti ya Leo Jumapili ya Februari 21

Ofisa Mipango Na Aliyekuwa Mgombea Urais Zanzibar


Chama cha ACT Wazalendo kimemsimamisha uanachama Ofisa Mipango wake, Ali Makame Issa kwa madai ya kukiuka maadili ya chama hicho.

Wata Watatu Watiwa Mbaroni Kwa Kuvamia Kituo Cha Polisi Na Kuvunja Mlango Ili Kuwatoa Wenzao

Watu watatu wamekamatwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuvamia Kituo cha Polisi cha Duthumi na kuvunja mlango kwa lengo la kuwatoa wenzao watatu wanaotuhumiwa kwa wizi wa mifugo.

MIKAELA PROFESSIONAL TAILORS WAPANIA KUWAINUA WABUNIFU WA MAVAZI JIJINI MWANZA.

Idda Adam ambae ni Mkurugenzi wa Mikalea Professional Tailors ambao ni Mabingwa wa Ushonaji wa Mavazi ya aina mbalimbali Jijini Mwanza, akionyesha mavazi mbalimbali yanayopatikana ofisini kwake, Mtaa wa Ghana GreenView, Nyamanoro Jijini Mwanza.

KATIBU MKUU BAWACHA AZINDUA RASMI OFISI MPYA YA MBUNGE WA VITI MAALUMU MKOANI MWANZA.

Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema Taifa BAWACHA na Mbunge Viti Maalumu Taifa Grace Tendega (katikati) jana February 20,2016 akizindua ofisi Mpya ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza Chadema, Susan Masele (Kulia). Kushoto ni Paschazia Renatus ambae ni Katibu wa Bawacha Mkoa wa Mwanza.

BENKI YA POSTA TANZANIA YAJENGA VYOO VYENYE THAMANI YA SH. MILIONI 4.7 KATIKA SHULE YA MSINGI MAKAMBI ILIYOPO MANISPAA YA SONGEA MKOANI RUVUMA

 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Makambi iliyopo Kata ya Ndilima Litembo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifurahia vyoo vya kisasa vilivyojengwa na Benki ya Posta Tanzania.

NAFASI MBILI ZA KAZI ZINAHITAJI WATU WA KUZIJAZA HARAKA SANA. MSHAHARA NI MNONO PIA.

WANAHITAJIKA WAFAKAZI WAWILI WA KIKE NAFASI YA MAPOKEZI KATIKA HOTEL YA "MIGRATION LODGE" ILIYOPO SERENGETI MKOANI MARA. 

SIFA KUU NI KUJUA KUZUNGUMZA LUGHA YA KIINGEREZA KWA UFASAHA.

MSHAHARA WAO NI MZURI HIVYO PIGA SIMU 
0787 230 782 HARAKA KWA AJILI YA MAELEZO ZAIDI. MWISHO LEO.

OFISI YA MBUNGE WA VITI MAALUMU (CHADEMA) MKOANI MWANZA KUZINDULIWA RASMI HII LEO.

Viongozi mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ngazi ya Mkoa na Taifa hii leo wanatarajia kuzindua Rasmi Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) iliyopo Mtaa wa Ghana, Kata ya Nyamanoro Jimboni Ilemela.

WAKULIMA BUTIAMA MKOANI MARA WAPATIWA MAFUNZO YA KUPASHANA HABARI ZA KILIMO KWA NJIA YA SIMU

Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi (kulia), akizungumza na wakulima na Washiriki wa Mafunzo ya kutumia simu za mkononi kupashana habari za kilimo yaliyofanyika Kijiji cha Kisamwene wilayani Butiama mkoani Mara leo mchana.

29 DAYS TO GO; LADY JAYDEE OFFICIAL COUNT DOWN #NaamkaTena (VIDEO)

Lady Jaydee
Mkongwe wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee ametangaza rasmi kurudi tena kwenye muziki baada ya ukimya wa muda kidogo kwenye muziki. Lady Jaydee ameweka wazi ujio wake mpya kwenye muziki ikiwa leo ni siku ya 29 kuelekea uzinduzi wa #NaamkaTena. Tazama promo ya siku ya 29 ambapo Mh. Nape Nnauye kamzungumzia Lady Jaydee hivi.
"Mimi Kama kiongozi wa Sanaa nchini, Nitahakikisha natetea muziki wa Tanzania Lady JayDee anaamka tena", amesema Mh.Nape Nnauye.
#LadyJayDeeOfficialCountDown #NaamkaTena

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More