wakati baraza la Sanaa nchini (BASATA) limetoa taarifa kwa vyombo vya habari kuzuia kupigwa kwa wimbo wa msanii Ney wa Mitego anayeshukiliwa na jeshi la Polisi kutokana na wimbo huo
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.
Waziri wa habari, utamaduni na michezo Dkt Herrson Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.
Akiongea na Wandishi wa Habari muda huu mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO, na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile Wakwepa Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga, Wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.
Kutokana na mkanganyiko huu ni wazi Ney wa Mitego kashawanasa BASATA yawezekana kwa kukamatwa kwake lolote linaweza tokea
Monday, March 27, 2017
NEY WA MITEGO AWANASA BASATA, WAO WAFUNGIA WIMBO RAIS MAGUFULI ASEMA RUKSA KUPIGWA
Monday, March 27, 2017
mwangaza wa hbari
No comments
0 comments:
Post a Comment