OFISA
Tathimini na Ufuatiliaji wa Shirika la MMADEA kupitia mradi wa afya
bora kwa ustawi wa jamii, Hezron Kalolo amewataka viongozi wa serikali
za kijiji na wananchi kwa ujumla kujenga mazoea ya kuweka akiba ya fedha
zitakazowasaidia pindi wanawake wanapo karibia kujifungua na baada ya
kujifungua badala ya kusubiri serikali.
Alisema
kuwa pamoja na changamoto zilizopo zinazowakabili wananchi wa vijiji
mbalimbali, lakini shirika la MMADEA linatoa elimu juu ya afya ya uzazi
na madhara ya mimba za utotoni katika vijiji kumi na moja (11) vya
mradi.
Hezron
alisema haya jana kuwa mradi huo unatekelezwa katika kata za Idete,
Nyanzwa na Ibumu kupitia ufadhili wa shirika la Foundation for Civil
Society (FCS), huku wakifanya kampeni ya kuibua uelewa wa watu juu ya
changamoto za sekta ya afya.
Alisema
kuwa Wilaya ya Kilolo ni moja ya wilaya ya Mkoa wa Iringa yenye
changamoto ya mimba za utotoni na ndoa za utotoni ambapo wasichana wengi
hupata mimba kabla yakifikisha miaka 18.
Aidha,
Afisa Tathimini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la kiserikali la
MMADEA huyo alizitaja baadhi ya visababishi vya mimba za utotoni kuwa ni
kiwango kidogo cha elimu ya uzazi, umaskini, tamaa, ngono zembe,
shinikizo rika, ndoa za utotoni na utamaduni.
Kwa
upande wao, wananchi wa Kijiji cha Idete wilayani Kilolo, mkoani Iringa
wameiomba serikali kuwajengea zahanati kwa ajili ya kuweza kuboresha
huduma za afya ya uzazi kijijini hapo.
Walisema
kijiji hicho hakina zahanati ya serikali kunakopelekea kuongezeka kwa
vifo vya wajawazito na watoto vitokanavyo na uzazi, kumbe kungekuwepo na
zahanati ya serikali huduma za afya zingetolewa kwa gharama nafuu
kupitia mfuko wa bima ya afya ya jamii (CHF).
Wakizungumza
jana katika nyakati tofauti wakati wa mkutano wa hadhara, wananchi hao
walilipongeza shirika lisilo la kiserikali la Mazombe Mahenge
Development Association (MMADEA) la mkoani Iringa kwa kutoa elimu ya
masuala ya afya ya mama na mtoto, huku wakisema kumekuwa na hali
yasintofahamu katika kutetea afya zao.
Walisema
kuwa wanatumia gharama kubwa za huduma za afya kutokana na zahanati
iliyopo ambayo sio ya serikali kutoza gharama kubwa za matibabu na
kuongeza kuwa kungekuwepo na zahanati ya serikali gharama hizo zingekuwa
nafuu.
Wananchi
hao walisema kuwa wamekuwa wakilazimika kutembea mwendo mrefu kutoka
Kijiji cha Idete hadi Kituo cha Afya cha Kidabaga kilichopo katika kata
nyingine wilayani kilolo, mkoani Iringa.
Walisema
kuwa kukosekana kwa kituo cha afya katani kwao ni sababu inayopelekea
wananchi hao kutembea kwa mwendo mrefu kufuata huduma ikichangia na
miundombinu mibovu ya barabara, ambapo magari mengi yanashindwa kufika
na kulazimika kukodi gari ya kanisa katoliki kwa gharama kubwa kutokana
na kutokuwepo gari la wagonjwa katika zahanati ya inayomilikiwa na
kanisa la KKKT.
Walisema
kuwa kungekuwepo na mfuko wa afya wa CHF kungesaidia katika kupunguza
gharama za huduma za afya huku wa kihoji kwanini wachangie gharama kubwa
ya gari ya wagonjwa kutoka halmashauri wakati serikali inatoa huduma
bure za afya ya uzazi.
Wananchi
hao wa Kijiji cha Idete, wilayani Kilolo mkoani Iringa wapo hatarini ya
kukumbwa na changamoto ya kuwapoteza wanawake wajawazito na watoto
kutokana na umbali wa kituo cha afya, huku wakilazimika kuchangia gari
la wagonjwa kutoka halmashauri na la kanisa katoliki.
Tumpe
Mwadisa ni mkazi wa Kijiji cha Idete, akiongea na mwandishi wa habari
wa Nipashe wakati akishuhudia akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Iringa ya
Rufaa ambako alikwenda kujifungua kwa kupata msaada wa gari la
halmashauri lililofika kijijini hapo kwa shughuli zingine.
Alisema
kuwa changamoto ya kuwapoteza wanawake wajawazito na watoto inatokana
na kutokuwepo zahanati ya serikali na kituo cha afya kwa kata nzima ya
Idete.
Kwa
upande, wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Idete, Bimas Mkemwa pamoja na
Diwani wa Kata ya Idete Bruno Kauku wamesema kuwa elimu inayotolewa na
shirika la MMADEA imewafungua kwa kiasi kikubwa wananchi, kwani hawakuwa
na elimu ya kutosha juu ya mfuko wa afya jamii na upatikanaji wa huduma
za afya ya uzazi. huku wakiiomba serikali kuwajengea zahanati ili
kunusuru maisha ya mama na mtoto.
Kufuatia
hali hiyo wakazi na viongozi wa Kijiji cha Idete katika kata Idete,
wilayani Kilolo mkoani Iringa wameiomba serikali kusaidiana kujenga
zahanati ili waweze kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu hususan
wajawazito ya kufuata huduma za afya.
Hata
hivyo, wananchi wamelia na viongozi wa kitaifa kutofika kijijini hapo
kwa miaka mingi ili kujionea adha wanazozipata wananchi wa kijiji hicho
pamoja na kijiji hicho kuwa ni makao makuu ya kata.
0 comments:
Post a Comment