Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)imeiagiza
Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa kuboresha barabara zake za pembezoni
mwa mji ili zitoe huduma kwa wananchi.
Akizungumza
wakati wa majumwisho wa ziara ya siku moja ya kamati kwenye Manispaa ya
Iringa jana makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Abdallah Chikota alitoa
maelekezo kuboresha miundombinu ya barabara pembezoni mwa mji.
Alisema
kuwa Manispaa ya Iringa imeelekeza nguvu kubwa katikati ya mji na
kusahau barabara za pembezo ambazo zitasaidai kutoa huduma kwa wananchi.
Chikota alisema kuwa wananchi walioko pembezoni mwa mji ni sawa na wananchi wa katikati ya mji.
Kuna
tofauti kubwa kati ya wananchi waishio pembezoni na katikakti. Barabara
za pembezoni mwa mji hazina kiwamgo vya ubora…,” alisema Chikota.
Aidha,
Kamati ya Kudumu ya Bunge za Hesabu za Serikali za Mitaa ilitembelea
barabara za Mkimbizi- kihesa Sokoni-Tumaini Univesrsity and Ngome na
kukuta havian vivuko kwa kurahisha wananchi kufika kwa krahisa katika
makazi yao.
Alisema
kuwa barabara hizo pamoja na kukamilika ujenzi wake zilikuwa hazina
baadhi ya alama za barabarani na vivuko vya watembelea kwa miguu.
Hatua
hiyo imetokana na ujenzi wa barabara wa hizo kutokuwa na baadhi ya
miundombinu vikiwemo vivuko vya kufanya barabara hiyo kutokuwa rafiki
kwa mwananchi.
Mradi
wa ujenzi wa barabara unajumuisha vipande vitatu vya barabara za
Mkimbizi TBA (1.10km), Kihesa Sokoni-University of Iringa (zamani
Tumaini University (0.70km) na Ngome–Mwang’ingo (0.45km) uliyobuniwa ili
kuinua kiwango cha barabara hizi kutoka changarawe hadi kiwango cha
lami.
Halmashauri
ya Manispaa ilifanya matengenezo ya barabara hizi kwa kiwango cha lami
kwa kutumia fedha za mfuko wa barabara (Road Fund) kwa bajeti ya mwaka
2013/2014 ambazo zilivuka mwaka.
Akitoa
taarifa kwa kamati Mhandishi wa Ujenzi wa Manispaa ya Iringa, Mashaka
Luhamba alisema kuwa mradi huo ulianza kutekeleza tarehe 1/11/2013 na
uilikamilika tarehe 18/09/2014.
Alisema kuwa kazi hiyo ilitekelezwa na Mkandarasi G’S Contractors kwa mkataba wa gharama ya 1,088,505,000/-.
Luhamba
alisema kuwa kazi hiyo ililenga na pia kupunguza kero kwa wananchi wa
eneo la mkimbizi ambalo halina barabara ya uhakika na lina wakazi wengi.
Naye,
Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu alisema amepokea maagizo
hayo kutoka kamati ya kudumu ya bunge za hesabu za serikali za mitaa
(LAAC)na kuahidi kuyafanya kazi mapendekezo hayo.
Wamoja
alisema kuwa kupitia sekritarieti ya mkoa atahakikisha wanasimia
utekelekezaji wa maagizo kwa manispaa ya iringa yanafanyika.
Kamati
ya kudumu ya bunge za hesabu za serikali za mitaa (LAAC) ilitembelea
miradi mbalimbali hapa manispaa ya iringa ikiwemoile ya maji, barabara
na machinjio ya kisasa ambao hata hiyo mradi huo umechukua muda mrefu
kukamilika (miaka kumi).
Pia
kaamti hiyo imeagiza watendaji wa Manispaa ya Iringa kusimamia miradi
hiyo inayotumia gharama za walipa kodi kwa kuzingatia viwango wa ubora.
0 comments:
Post a Comment