Wednesday, March 29, 2017

WAKURUGENZI NCHINI WACHAGUA VIONGOZI WAO MD KAYOMBO JOHN AWA MUWEKA HAZINA

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA wa Wakurugenzi nchini
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba, ambaye kachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Wakurugenzi nchini
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Ndg Anne Claire Shija (Kushoto) ambaye kachaguliwa kuwa katibu wa Wakurugenzi nchini

Na Mathias Canal, Dodoma

Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya na Manispaa kote nchini kwa kauli moja wameridhia na kuwachagua viongozi watakaowawakilisha katika kufikisha changamoto zao mbalimbali katika ngazi za juu ili kupungunza uwasilishaji wa kila Mkurugenzi kufikisha changamoto zake ngazi za juu.

Uchaguzi huo umefanyika hii Leo katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma kwa maridhiano ya Wakurugenzi wote kwa asilimia 100% ya kura zote.

Uchaguzi huo umejili Mara baada ya kumalizika kikao cha kazi kilichoongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Eng Musa Iyombe kilichohudhuriwa na Wakurugenzi wote 185.

Wakurugenzi hao wamefanya uchaguzi kwa nafasi nne ambazo ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti sambamba na Katibu pamoja na Muweka Hazina.

Wakurugenzi waliochaguliwa katika nafasi hizo ni

1. Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Ndg Kiomoni Kibamba, ambaye kachaguliwa kuwa Mwenyekiti

2. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Ndg Rachel Chuwa ambaye kachaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.

3. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Ndg Anne Claire Shija, ambaye kachaguliwa kuwa katibu. Na

4. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Ndg John Lipesi Kayombo ambaye kachaguliwa kuwa MUWEKA HAZINA

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Mara baada ya uchaguzi huo kumalizika Viongozi hao waliochaguliwa wameeleza namna bora ya kuhumiza uwajibikaji kwa Wakurugenzi wote sambamba na kuwawakilisha vyema kufikisha changamoto zao kwa ngazi za juu.

Wameueleza mtandao wa www.wazo-huru.blogspotm.com kuwa imani kubwa waliyopatiwa na Wakurugenzi wote nchini ya kuwachagua kuwa wawakilishi wao ni kubwa hivyo wana kila sababu ya kuitumikia kwa weledi na usawa.

"Kupitia Wawakilishi hao waliochaguliwa Wakurugenzi nchini wataraji utendaji uliotukuka na uwakilishi unaostahili kulingana na changamoto zinazowakabili katika maeneo yao" Alisema MD Kayombo John L.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More