Mahakama
Kuu imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Wakili Onesmo
Mpinzila pamoja na mambo mengine akipinga Kanuni za Uchaguzi za Chama
cha Wanasheria Tanganyika (TLS) za mwaka 2016.
Kesi
hiyo imetupiliwa mbali baada ya Mahakama kukubaliana na hoja za
mapingamizi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ndio waliokuwa
wadaiwa katika kesi hiyo.
Hoja
hizo ambao Mahakama imekubaliana nazo ni pamoja na kwamba mdai hakuwa
na mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo na kwamba hati yake ya kiapo
kilichokuwa kikiunga mkono madai yake ilikuwa na kasoro za kisheria.
Uamuzi
huo umesomwa na Jaji Ignasi Kitusi kwa niaba ya jopo la majaji watatu
waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo. Majaji wengine walikuwa ni Rose
Teemba(kiongozi wa jopo) na Beatrice Mutungi.
0 comments:
Post a Comment