Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe akizungumza na waandishi wa habari Mkoani iringa
HALIMASHAURI ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa imewasainisha mikataba wakandarasi 14 kwa ajili ya matengenezo ya barabara mbali mbali za mji wa Iringa .Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Alex Kimbe akizungumza leo kabla ya zoezi la kuwasainisha mikataba hiyo alisema kiasi cha Shilingi bilioni 1,389,455,041.20 kimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo .
Alisema kuwa halmashauri yake imeendelea kutekeleza miradi mbali mbali ya matengenezo na ujenzi wa barabara kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kupitia fedha za mfuko wa barabara.
"Kazi zinazokusudiwa kufanyika ni matengenezo ya muda maalum (Periodic maintenance works) ikihusisha ujenzi wa barabara ya lami ya Frelimo -Muungano (Routine maintenance works) na ujenzi / ukarabati wa madaraja "
Alisema kuwa mchakato wa kuwapata wakandarasi kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo ukifanyika kwa mujibu wa sheria ya manunizi ya umma ya mwaka 2011 na kanuni zake na kuwa zabuni za ushindani kitaifa zilitangazwa katika magazeti na website za zabuni ya mamlaka ya uthibiti wa manunuzi ya umma hivyo alitaka wakandarasi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Kimbe aliwataka wakandarasi hao kuanza utengenezaji wa barabara hizo na kuwa Manispaa haitasita kusitisha au kuvunja mkataba kwa mkandarasi atakaye fanya kazi chini ya kiwango.
Kuwa kukamilika kwa miradi hiyo ya barabara kutarahizisha usafiri wa uhakika katika maeneo mbali mbali ya mji wa Iringa ambayo wananchi wake walikuwa wakisumbuka na adha ya usafiri kutokana na ubovu wa miundo mbinu.
"kwa barabara kuboreshwa tutaboresha usafi wa mazingira, kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Iringa pia kurahisisha utoaji na usimamizi wa huduma za jamii kama elimu na afya "
Alisema kazi zitakazofanywa ni utengenezaji wa barabara ya kiwango cha lami Barabara ya Frelimo,na Muungano pia matengenezo ya kawaida ya barabara za kata za Mtwivila, Nduli, Mlandege, Mshindo, makorongoni, Kitanzini Isakalilo, Mvinjeni, Gangilonga, Ilala, Kitwilu, Ruaha, mkwawa, Mkimbizi, Kihesa na maeneo mengine ya mji wa Iringa.
0 comments:
Post a Comment