hilo bango lina maneno ambayo tulikuwa tunaamini kuwa uongozi wa lipuli na wanachama wote wanapenda mpira na sio majungu lakini kinachoendelea saizi ndani ya club ya lipuli tofauti na hilo bago
Wadau wa soka mkaoni iringa bado wapo
njia panda juu ya maandalizi ya timu ya lipuli kutokana na mgogoro uliopo baina
ya kamati tendaji ya timu hiyo na Abu Changawe Majeki aliyefunguliwa na chama
cha soka mkoa wa iringa.
Wakizungumza na blog hii wadau hao
walisema kuwa timu ya lipuli inahalibiwa
na viongozi wachache walevi wa madaraka na pesa ambazo zitapatikana kutokana na
lipuli kupanda hadi ligi kuu.
Msomali ni mmoja wa wajumbe wa
kamati tendaji ya lipuli ambaye alisema kuwa ukitaka kuwa kiongozi ndani ya
timu ya lipuli ni lazima upatane na Abuu Majeki au willy Chikweo hapo utakula kiulaini
ila usipopatana na hawa viongozi basi wewe utageuka kuwa adui namba moja.
“Mimi ndio nahusika kutoa pesa bank
za lipuli ila kiukweli Majeki na Chikweo ni waroho wa madaraka hasa linapokuja
swala la pesa,hatuwezi kuendesha timu tukiwa na viongozi hawa wawili ni
wanafiki na wanauchu wa madaraka mimi sipendi hivyo napenda mpira wa miguu
uchezwe hapa nyumbani(Iringa)”alisema Msomali
Kwanini sasa wadau wanawalaumu na
kuwatupia lawama viongozi hawa wawili Abu Changawe Majeki na Wille Chikweo?
Abu Changawe Majeki alisema kuwa lipuli ni timu
ya wanachama hivyo ni lazima tufanye uchaguzi ili tupate viogozi wenye uwezo wa
kuendesha timu ya ligi kuu na sio kubaki na viongozi wasio na sifa ya kuendesha
timu ya ligi kuu.
“Mimi binafsi nimerudi kuja
kusimamia uchaguzi ili tupate viongozi wenye uwezo wa kuongoza timu ya ligi kuu
lakini bila kujua nini tatizo najikuta nimefungiwa na wanaojiita kamati tendaji
wakati kama hiyo hawana mamlaka ya kunifungia” alisema Majeki
Majeki alisema kuwa viongozi wa lipuli wengi hawataki
tuwe na wanachama wapya ndio maana hata kadi wamezificha majumbani kwao sasa
hiyo ni aibu kubwa,kwanini hawataki tuwe na wanachama wapya.
“Haiwezekani timu ikawa na wanachama
walewale kila siku ni lazima tufanye jitihada za kuongeza wanachama lakini
kwanini wakina Chikweo na kundi lake hawataki na wanaweka masharti magumu
kupata wanachama wapya na kwanini hawataki kunitambua kuwa mimi kiongozi wao
wakati adhabu yangu imeisha?” alisema Majeki
Naye katibu mkuu wa timu ya lipuli
Wile Chikweo alisema kuwa wamemfungia Majeki kutokana na kuvunja katiba ya timu
ya lipuli kwa kuwapiga baadhi ya viongozi,wajumbe na wanachama wa timu ya
lipuli.
“Mimi nishapigwa na majeki na ameshapiga
viongozi wengine na kuna baadhi ya wananchama walishampeleka mahakamani
kutokana na ubabe wake hivyo hapaswi kuwa kiongozi wa lipuli hata siku moja”alisema
chikweo
“Wakati Majeki kafungiwa kulikuwa kumetulia
na ndio maana tulifanikiwa kupandisha timu lakini hatujui njia gani ilimasawa kumfungulia
Majeki wakati akiwa kwenye adhabu yake alikiuka mambo mengi ya adhabu hiyo
mfano alijihusisha na mashindano ya msofe Cup” alisema Chikweo
Kuna mdau mmoja ambaye hakutaka jina
lake liandikwe hapa alisema kwanini chama cha mpira manispaa kimekaa kimya na
kwanini chama cha mpira kimekaa kimya,basi ujue kuwa Chikweo bado anafitna na
baadhi ya viongozi kutokana na uchaguzi uliopita na ndio maana kuna makundi
mawili, kundi moja linamsaidia majeki na kundi lingine lipo pamoja na kamati
tendaji ya lipuli na ndio linalotoa maagizo yote hivyo naomba viongozi wa
wilaya kam mkuu wa wilaya Richard Kasesela na Mkuu wa mkoa Bi Amina Masenza
kuingilia kati mgogogoro huo.
Hivi ni kweli malkia wa lipuli madam Jesca msambatavangu,mwemyekiti wa mipango na fedha wa lipuli jully
sawani,katibu wa lipuli fc lonjino malambo, katibu wa IRFA ally ngalla,Mjumbe wa mkutano mkuu TFF abuu silia, Mwemyekiti wa Chama cha Soka Manispaa ya iringa lupyana masawa, mwakilishi wa vilabu manispaa Michael Mlowe na mjumbe wa kamati tendaji IRFA david wapalila
mnashindwa kuwaita Majeki na Chikweo mkazungumza nao ili kumaliza mgogoro huu.
0 comments:
Post a Comment