Mkuu wa shuleya Ngoti Green Academy Jonson Mtewele kushoto akiwa na mkurugunzi wa Ngoti Green Academy Thomas Ngoti ambaye alikuwa anatoa neno kwa wazazi waliofika kwenye kikao cha pamoja baina ya wazazi walimu na wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo
Mmoja wa wazazi walifika katika shule ya Ngoti Green Academy akitoa neno mbele ya wageni waalikwa na mkurugunzi wa Ngoti Green Academy Thomas Ngoti
Picha za pamoja baina ya wazazi,walimu na viongozi wa shule ya Ngoti Green Academy
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Ngoti Green Academy
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
Mkuu
wa shule ya Ngoti Green Academy
amewataka wazazi na walezi mkoani Iringa kuwalea watoto katika maadili
yanayostahili ili kuwa na kizazi chenye maadili na uwajibikaji kwa jamii na
kuleta maendeleo ya nchi na familia zao.
Akizungumza
na wazazi wa shule ya Ngoti Green Academy mkuu wa shule hiyo Jonson Mtewele alisema
kuwa maadali ya mtanzania yanazidi kupotea kutoka na mmong’onyoko wa utandawazi
“Mimi
nasema kuwa saizi tamaduni za kimagharibi zimeharibu sana utamaduni wenu maana
wananchi wengi wanaiga bila kujua wanaiga maadili gani ndio maana saizi watoto
wetu wengi wamekuwa hawana maadili” alisema Mtewele
Mtewele
aliwataka wazazi kuacha kuwafundisha tamaduni za kimagharibi ambazo hazina
maadili ya kimaendeleo kwa watoto wadogo ambao ndio wamekuwa waathirika wakubwa
kwenye hizi tamaduni za kimagharibi.
“Mtoto
kutoka mwaka mmoja hadi miaka nane ndio umri wa mtoto kupokea vitu vipya
kichwani mwake ndio maana nasema ukikosea kumlea mtoto katika umri huo basi
waweza kulea mtoto akiwa hana maadili yatayomuwezesha kufanikiwa katika maisha
yake” alisema Mtewele
Aidha
Mtewele alisema shule ya Ngoti Green Academy inawafundisha wanafunzi katika
mfumo wa maadili ya dini kutoka na matendo ya bwana yesu aliyaonyesha duniani
na kuwa mfano wa maadili bora.
“Tunataka
mtoto akue katika maadili ya kikristo kwa maana kuwa tunamtaala wenye tabia
njema siti ambazo bwana yesu alizionyesha akiwa duniani upole,unyenyekevu na
wakati furani kukubali kuonewa na sio lazima abishe kila kitu na
tunavyomuelekeza kwa namna hivyo tumegundua kuwa watoto watakuwa kati hali
hiyo” alisema Mtewele
Mtewele
aliongeza kuwa shule hiyo inapokea watoto kuanzia mwaka mmoja hadi miaka nane
kwa kuwa huo ndio wakati mzuri wa kuwalea watoto kimaadili na kuwajengea uelewa
wa maisha ya baadae.
“Tumeruhusiwa
kuwapokea watoto kuanzia umri wa mwaka mmoja hadi miaka nane baada ya hapo
inakuwa vigumu kupokea watoto wa zaidi ya miaka hivyo kwa mjibu ya mtaala ambao
tunao” alisema Mtewele
Naye
mkurugunzi wa Ngoti Green Academy Thomas Ngoti alisema kuwa shule hiyo inatoa
elimu iliyobora ambayo inatakiwa kitaifa na kimataifa kutokana na mtaala ambao
wanautumia.
“Ngoti
Green Academy inatoa elimu kwa upana wake ndio maana wazazi wengi wameanza
kuwaleta watoto wao hapa kwa ajili ya watoto wao kupata elimu bora ambayo inapatika
hapa nadio huo ubora wake” alisema Ngoti
Ngoti
aliongeza kuwa wanampango wa kwenda kwenye ngazi ya sekondari na chuo kikuu kwa
kuwa wamekuwa wakitoa elimu iliyobora hivyo hata serikali inawaamini kwa kuwa
wanamtaala mzuri wa kutoa elimu bora kwa wanafunzi ambao watakuwa wanasoma
kwenye sekondari na chuo kikuu.
“Ngoti
Green Academy Thomas ni chombo kamili cha kuandaa watoto wadogo ambao bado
hawajalishwa vitu vingi kichwani na ndio maana wanataka kuanziasha sekondari na
chuo kikuu ili wanafunzi weweze kupata elimu bora kwa mtaala bora ambao
wanautumia” alisema Ngoti
Ngoti
alisema kuwa Ngoti Green Academy inapatikana maeneo ya Mtwivila sehemu inaitwa
Mwambusi au unaweza kutembelea makao mkuu ya kampuni yalipo jingo la IMUCU
gorofa namba moja chumba na kumi na nane lakini unaweza kupiga namba 0765800310
au 0718056561 hapo ndio itakuwa kazi rahisi kuwapata.
0 comments:
Post a Comment