Serikali imepiga marufuku watu kufunga ndoa bila kuwa na cheti cha kuzaliwa kuanzia Mei Mosi, mwaka huu.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hayo leo akiwa
katika ziara yake mkoani Morogoro na kuongeza kuwa serikali imeamua
kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia
kupanga mipango ya kimaendeleo sanjari na kuzuia wageni kuingia
kinyemela nchini.
Pamoja
na mambo mengine, Dk.Mwakyembe amewataka Wakala wa Usajili wa vizazi na
Vifo (RITA), kuhakikisha inasimamia sheria ya usajili ambapo amesema
kuwa bila kuwa na takwimu sahihi za vizazi na vifo ama ndoa
inasababisha nchi kushindwa kusonga mbele kimaendeleo.
“Wenzetu
nchi zilizoendelea suala la usajili wamelipa kipaumbele lakini sisi
bado tuko nyuma, kwa mfano Mkoa wa Morogoro kwa mujibu wa sensa ya
watu na makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuna jumla ya wakazi milioni
2.2, lakini waliosajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa ni asilimia 11
pekee huku wengine wakiwa bado hawasajiliwa,” amesema.
0 comments:
Post a Comment