Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule akizungumza na viongozi wa Kijiji na Kata ya Gonja Maore na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa Wilaya
Dc Senyamule akishiriki zoezi la kupanga matofali yaliyofyatuliwa na wananchi wenyewe kwa ajili ya miradi ya maendeleo Wilayani humo.
Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Mhe Rosemary Staki Senyamule ametenga Siku moja katika Juma ili kushiriki shughuli za maendeleo kwa kushirikiana na wananchi.
Huu ni utaratibu ambao Mkuu huyo wa Wilaya ameuanzisha kwa muktadha wa kuchochea ari katika utendaji Kazi na uwajibikani kwa kila mwananchi ili kuimarisha na kusukuma kwa vitendo juhudi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa vitendo na utekelezaji wa utendaji kazi ili kuakisi dhana nzima ya serikali hii ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu.
"Nimeamua kutenga siku hii ya jumatatu kwani naamini italeta hamasa kwa wananchi kupenda kazi za maendeleo, itawatia moyo na kuona kuwa serikali ipo karibu nao ". Alisema Staki
Akizungumzia kuhusu kuanza kwa vitendo utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Dc Staki amesema kuwa asilimia kubwa ya watanzania wanaoishi kwa mazoea ya kuyumbishwa na siasa zisizo na manufaa kwao lakini huu si wakati tena wa kurudi nyuma badala yake watanzania wote wanapaswa kushirikiana katika kufanya Kazi na kulifanya Taifa Letu kufika mbali zaidi kimaendeleo.
Hii imekuwa ziara ya mwanzo ya Mkuu huyo wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki kwa kushiriki kufanya kazi za Jamii akiwa na dhamira ya kuwatia Moyo wananchi ili kupunguza lawama zisizo na lazima kwa serikali na badala yake kujituma katika kufanya kazi.
Ziara hiyo katika kushiriki Kazi za jamii imefanyika katika kijiji cha Mheza na Maore vilivyopo kata ya Gonja Maore huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kuishauri na kushirikiana na serikali.
Kwa upande wawananchi wa maeneo hayo walionyesha kufurahishwa na utaratibu huo ambao haujawahi kufanyika na kiongozi yeyote katika Wilaya ya Same tangu kuumbwa kwa msingi ya ulimwengu.
Wananchi hao wamemuakikishia Mkuu hiyo wa Wilaya hiyo kuwa watashirikiana nae katika shughuli za maendeleo kwani kwa kiasi kikubwa udini na uzembe wa watendaji wengi umesababisha kuendelea kuzorota kwa maendeleo ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Pamoja na hayo pia Dc Staki Ametoa onyo kwa wananchi hususani Vijana ambao ni wavivu katika kushiriki shughuli za Jamii kuchukuliwa hatua Kali za kinidhamu kW kila mwananchi atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake.
0 comments:
Post a Comment