WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa siku 14 kwa maofisa
wanaohusika na udhibiti wa dawa za kulevya kwenye mpaka wa Tunduma mkoa
wa Songwe, kuwakamata watu wanaohusika na uvushaji wa dawa hizo kutoka
nchini kwenda nchi jirani ya Zambia na nyingine zilizopo ukanda huo.
Nchemba
alitoa agizo hilo jana, alipofanya ziara ya kukagua mpaka huo, ambapo
alisema ni jambo lisilofichika kuwa kwa sasa Tanzania imechafuka
kutokana na dawa za kulevya.
Alisema
kutokana na Watanzania wengi kukamatwa katika nchi mbalimbali duniani,
wakijihusisha na usafirishaji wa dawa za kulevya, imefikia hatua kwa
baadhi ya nchi kufikiria kuongeza masharti zaidi kwa kila
atakayejitambulisha kuwa Mtanzania.
“Hatuwezi
kuacha nchi ikachafuka kwa sababu tu ya watu wachache.Ukienda China
Watanzania zaidi ya 200 wanashikiliwa kwa dawa za kulevya, Pakistan
wapo, India, Afrika Kusini ni Watanzania. Hili linatuchafua sana,” alisema Nchemba.
Aliutaja
mpaka wa Tunduma kuwa miongoni mwa maeneo yanayoongoza kwa kupitisha
dawa hizo na kutaka nguvu kuongezwa zaidi ili kuwezesha misako.
Alisema
wapo watu ambao si makondakta wa mabasi wala abiria, lakini wamekuwa
wakisafiri kila siku kwenye mabasi, hatua inayodhihirisha kuwa ndiyo
wanaojihusisha na usafirishaji wa bidhaa hizo haramu.
Alisema
watu hao wamekuwa na ushirikiano na watu wengine katika miji ya jirani,
kabla ya kufika mpakani ikiwemo kijiji cha Mpemba wilayani Momba mkoani
Songwe, ambapo wakifika hapo basi husimamishwa na mzigo kushushwa,
kisha kusafirishwa kwa njia za panya hadi ng’ambo ya nchi.
“Wakati
ninyi mnafanya utaratibu wa kawaida wa kupitisha gari husika hapa
mpakani, wao wanavusha kupitia njia za panya. Basi likishavuka na mzigo
unakuwa umefika Zambia wanakutana na kuupakia tena kisha wanaendelea na
safari.
“Na katika hili ni lazima mzungumze pia na wenzenu wa upande wa pili, wadhibiti pia mji unaofuata baada ya huo wa mpakani maana huko ndiko wanakopakia tena. Kama mtashindwa katika wiki mbili, nitakuja mimi mwenyewe na nitawakamata tu,” alisisitiza.
“Na katika hili ni lazima mzungumze pia na wenzenu wa upande wa pili, wadhibiti pia mji unaofuata baada ya huo wa mpakani maana huko ndiko wanakopakia tena. Kama mtashindwa katika wiki mbili, nitakuja mimi mwenyewe na nitawakamata tu,” alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment