Mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga, Moïse Katumbi, wakati wa mahojiano Lubumbashi, Juni 2, 2015.
Mwanasiasa
wa upinzania, ambaye aliwahi kuwa mshirika wa karibu wa Rais Joseph
Kabila, Moise Katumbi Chapwe, amesema anaunga mkono tangazo la muungano
wa vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa
“Rassemblement” na kuwatolea raia wito wa kusalia nyumbani Jumanne
Agosti 23.
Muungano
wa vyama vya upinzani wa “Rassemblement” unadai kuungwaji mkono Katiba
na uzingatiaji wa azimio 2277 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa;
Muungano huo pia unasema kuwa idadi ya wafungwa wa kisiasa ambao serikali imetangaza kuwachia huru haitoshi;
Vile vile muungano huo unalaani kuitishwa kwa Tume ya matayarisho ya mazungumzo na msuluhishi Edem Kodjo.
Muungano wa vyama vya upinzani wa “Rassembement umetolea wito raia kusalia nyumbani kwa siku ya Jumanne tarehe 23 Agosti.
Moise
Katumbi, katika tangazo alilolitoa Jumatatu jioni anasema ni muhimu kwa
kupinga ujanja wa serikali ambao unaonyesha wazi kuwa ni uonga wa
kisiasa, wakati ambapo imeendelea na mpango wake wa kuwakandamiza
kiholela wafuasi wa vyama vya upinzani na kushawishi vyombo vya sheria.
Moise
Katumbi Chapwe anasema kuachiliwa huru kwa watu wanne wasio kuwa na
hatia ni ujanja wa serikali wakati ambapo bado kuna mamia ya wanasiasa
wanaendelea kusalia katika magereza mbalimbali nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
Masharti
ya kushiriki katika mazungumzo yaliyotolewa na muungano wa vyama vya
upinzani wa "Rassemblement" wakati wa mkutano wa mjini Genval bado ni
vigumu kutekelezwa. Kuitishwa kwa Tume ya matayarisho ya mazungumzo na
Msuluhishi Edem Kodjo ni jambo lisilokubalika na ni uchochezi dhidi ya
raia wa Congo, amesema Moise Katumbi.
Kwa hiyo,
naitikia wito wa muungano wa vyama vya upinzani wa "Rassemblement" kwa
kusalia nyumbani kwa siku ya Jumanne, Agosti 23, 2016 nchini kote DRC.
Natoa witokwa raia wa Congo wanataka kudumisha demokrasia kusema HAPANA
kwa kusogeza mbele kalenda ya uchaguzi, ameongeza Bw Katumbi Chapwe. RFI
0 comments:
Post a Comment