MAHAKAMA
ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imewahukumu kutumikia kifungo cha
maisha jela vijana wawili wakazi wa wilayani Chunya mkoani humo kutokana
na kosa la ubakaji wa mwanamke mmoja waliyemtendea kitendo hicho mbele
ya watoto wake.
Kadhalika,
mahakama hiyo imewahukumu vijana hao wawili kutumikia kifungo cha miaka
30 jela kutokana na kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo siku
ya tukio walimjeruhi mume wa mwanamke waliyembaka.
Vijana
waliokumbwa na vifungo hivyo viwili kutokana na mashitaka mawili
yaliyokuwa yakiwakabili ni Ngaru Joseph (32) na Pili Mneme Kapigi (30)
wote wakiwa ni wakazi wa wilayani Chunya mkoani Mbeya.
Awali
ilielezwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka wa Jeshi la Polisi
Mazoya Luchagula, Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Alice
Mkasela kuwa mnamo Julai 10, mwaka huu saa nane usiku nyumbani kwa
mlalamikaji katika Kijiji cha Ukwavila wilayani Mbarali washitakiwa
walivamia na kuvunja mlango nyumba ya mkazi huyo aliyekuwa amelala na
mke na watoto wao.
Luchagula
alisema walipofanikiwa kuingia ndani ya nyumba hiyo washitakiwa hao
walimjeruhi baba wa familia kwa kumkata na shoka kichwani kisha wakapora
fedha kiasi cha Sh 580,000, wakachukua nguo zote za wanafamilia na
kisha kumbaka mama wa familia mbele ya mumewe na watoto.
Mwendesha
mashitaka huyo alisema wanafamilia hao kupitia mwanga wa taa ya sola
waliweza kuwatambua watuhumiwa kabla wazazi hawajapelekwa Hospitali ya
Misheni Chimala walikolazwa kwa ajili ya matibabu.
Kutokana
na makosa hayo Luchagula aliiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa
washitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine walio na tabia hizo
wilayani hapa na kwingineko nchini.
Akito
adhabu kwa washitakiwa, Hakimu Mkasela alisema ameridhishwa na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo na pande zote mbili na kwamba kwa kosa la
kwanza la unyangaji wa kutumia silaha washitakiwa watakapaswa kutumikia
kifungo cha miaka 30 jela na kwa kosa la pili la ubakaji watatumikia
kifungo cha maisha jela ili iwe fundisho kwao na watu wengine.
Awali
washitakiwa waliiomba Mahakama kuwapunguzia adhabu wakisema bado umri
wao ni mdogo na wanategemewa na familia zao, maombi ambayo yalitupiliwa
mbali na hakimu Mkasela.
0 comments:
Post a Comment