Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood
Mgimwa akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu akiwa sambamba na mwenyekiti wa ccm wilaya ya mufindi Yohanes Kaguo
na fredy mgunda,iringa.
Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa ameweza kugawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu za Jimbo hilo huku akitaka michezo yote kuendelezwa.
Mgimwa ametekeleza ahadi
hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Mufindi Kusini katika
ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa
kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.
Akielezea wakati wa kutoa
vifaa hivyo vya Michezo, Mgimwa amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni kutokana na ahadi yake yeye ka,a Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao
kuwapatia vifaa hivyo huku baadhi yao
pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.
“Niliahidi kuleta vifaa vya
Michezo kwa kila Kata. Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan
leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mgimwa.
Mgimwa ameongeza kwa kusema
ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za
kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
Amesema kuwa michezo licha
ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana
Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
Vifaa hivyo vya michezo
ikiwemo seti nzima za Jezi na mipira ya
kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao
wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.
Aidha, amewataka Vijana hao
kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya
vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha mpira wa
miguu kikiwa ni ajira kwao pia endapo michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana
walio pembezoni.
0 comments:
Post a Comment