WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Mkuu wa Idara ya Ardhi na
Miundombinu wa mkoa wa Rukwa pamoja na Ofisa Ardhi wa Manispaa ya
Sumbawanga kutatua matatizo ya ardhi yanayowakabili wakazi wa Manispaa
hiyo.
“Ijumaa
kuanzia saa 3.00 asubuhi wenye kero za ardhi wote waende kwenye ukumbi
wa Manispaa mkuu wa idara atakuwa na watumishi wote na hapa mtasikilizwa
kero zenu na kupatiwa ufumbuzi. Nasiku hiyo hakuna kazi nyingine ni
kusikiliza wananchi tu,” alisema.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 24, 2016) wakati
akizungumza na maelfu ya wakazi Mji wa Sumbawanga waliojitokeza katika
mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha Mandela katika jimbo
la Sumbawanga mjini ambapo aliwasisitiza watendaji hao kuwasikiliza
wananchi na kutatua kero zao.
Alisema
tangu alivyoanza ziara yake katika mikoa ya Rukwa na Katavi kila eneo
alilopita amekutana na wananchi wakiwa na mabango yanaeleza changamoto
na hii inatokana na viongozi wa mikoa hiyo kushindwa kutenga siku
maalumu kwa ajili ya kusikiliza kero hizo.
Waziri
Mkuu alibainisha kwamba baadhi ya mikoa na halmashauri mbalimbali
nchini zimeshaanza utaratibu huo wa kutenga siku maalumu katika wiki na
kusikiliza matatizo yanayowakabili wananchi jambo ambalo limeanza
kuonesha mafanikio ya utatuzi wa kero hizo.
Awali
akizungumza katika mkutano huo mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini
Aeshi Hilaly alisema wakazi wa Manispaa ya Sumbawanga wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ya migogoro mikubwa ya ardhi, hivyo
alimuomba Waziri Mkuu kuwasaidia katika kuipatia ufumbuzi.
Mbunge
huyo alisema migogoro hiyo ambayo imedumu kwa muda mrefu
imewasababishia usumbufu mkubwa wakazi wa jimbo hilo kukosa haki zao na
muda mwingi wamekuwa wakiutumia kufuatilia hatma ya ardhi yao bila ya
mafanikio hivyo kurudi nyuma kimaendeleo.
Pia
mbunge huyo alimuomba Waziri Mkuu kuwaondolea zuio la kuuza mazao yao
nje ya nchi kwa sababu kitendo hicho kimesababisha kushuka bei ya
mahindi na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima ambao wametumia gharama
kubwa katika kuandaa mashamba.
Akizungumzia
zuio hilo Waziri Mkuu alisema lengo la Serikali kuzuia uuzwaji wa mazao
nje ni kutaka kujiridhisha na uwepo wa chakula cha kutosha nchini ili
kuepuka kukumbwa na baa la njaa na kisha kwenda kuomba msaada kwenye
nchi tuliowauzia.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
0 comments:
Post a Comment