Watanzania
40,000 watanufaika kwa kupata ajira kwenye mradi wa ujenzi wa bomba la
mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Ajira
10,000 kati ya 40,000 zitakuwa za moja kwa moja na zilizobaki 30,000
zitatokana na watoa huduma mbalimbali wakiwemo mama ntilie au mama
lishe. Mradi huo ambao utazinduliwa Jumamosi ijayo na Rais John Magufuli
na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, utagharimu Sh trilioni nane (Dola za
Marekani bilioni 3.5) na utakamilika mwaka 2020.
Ili
kuhakikisha kuwa fedha hizo Sh trilioni nane zinawanufaisha zaidi
Watanzania, Jumuiya ya Watoa Huduma wa Sekta ya Mafuta na Gesi (ATOGS)
imepewa jukumu na serikali kuhakikisha kuwa inawaunganisha Watanzania
wote wanaotaka kuwekeza kwenye fursa mbalimbali zitakazoletwa na mradi
huo wa bomba.
Mmoja
wa waanzilishi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa ATOGS, Abdulsamad
Abdulrahim alisema kwa muda mrefu Watanzania wamekuwa wakibaki nyuma
kwenye miradi mbalimbali inayowekezwa nchini.
Abdulsamad
alisema kwamba lengo la ATOGS ni kuwaunganisha watoa huduma mbalimbali
kutoka sekta binafsi nchini kuchangamkia fursa za kibiashara kama vile
usafirishaji, uhandisi, ujenzi, bima, ulinzi, chakula, huduma za kifedha
za kibenki, vifaa vya ujenzi, huduma za kisheria na mawasiliano kwenye
mradi huo.
Naye
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dk Juliana Pallangyo
alisema Watanzania waache kulalamika na badala yake waungane na ATOGS
kuchangamkia fursa za kibiashara, na kutoa mwito kwa wananchi wa Tanga
na mikoa jirani kujitokeza kwa keshokutwa ambako Rais Magufuli na Rais
Museveni wataweka jiwe la msingi.
Kwa
upande wao, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)
walisema asilimia 80 ya ujenzi wa bomba hilo utafanyika Tanzania na
litapita kwenye mikoa nane ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Singida,
Tabora, Dodoma, Manyara na Tanga.
0 comments:
Post a Comment