Na Mathias Canal,
Lindi
Maonyesho ya Nanenane Kanda ya Kusini ambayo yalianza tokea
tarehe 1/8/2017 katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi yanaendela kushika kasi
huku kivutio kikubwa ikiwa ni baaada ya bidhaa mbalimbali zinazoonyeshwa kwenye
mabanda na Halmashauri mbalimbali kutoka mikoa yote miwili inayounda kanda ya
kusini ambayo ni Lindi na Mtwara.
Kwa ujumla wake maonyesho ni mazuri kwani yamehusisha
shughuli nyingi za Kilimo, Uvuvi na mifugo kama kauli mbiu inavyosema “Zalisha
kwa Tija Mazao na Bidhaa za Kilimo Mifugo na Uvuvi ili kufikia Uchumi wa Kati” kauli mbiu hii ikiwa na
msisitizo na hamasa zaidi kwa wananchi kutambua mbinu bora za Kilimo Mifugo na
Uvuvi ili kuwa na kipato kikubwa kitakachopelekea wananchi kwa ujumla wao
kufikia uchumi wa kati.
Pia kumekua na wajasiriamali wengi sana ambao wamefika
katika Maonesho hayo wakiwa na bidhaa mbalimali zikiwemo bidhaa za ngozi,
mikoba, viungo, asali, vyakula vya asili, mashine Ndogondogo na vingine vingi
vya kuvutia.
Maonyesho ya mwaka huu yamekua chachu na kuwa na mvuto
mkubwa kwani tangu kufunguliwa kwake kumekuwa na mgeni rasmi anayetembelea kila
siku ambao ni mwaaziri, ama wakuu wa mikoa kutoka katika mikoa husika jambo
ambalo limefanya maandalizi kuwa makubwa na mazuri zaidi.
Kanda ya kusini ina fursa nyingi za kiuchumi
kama vile Hali ya hewa nzuri, na Uzalishaji mazao mbalimbali hususani zao kubwa
la Korosho, Jambo la msingi ni kujipanga vizuri
na kuhakikisha tunatumia fursa hizi
kikamilifu ili kupunguza umasikini na kuleta utajirisho.
Katika hotuba nyingi zinazotolewa na wageni
mbalimbali wanaozuru katika Maonesho hayo ni kuhusu Tatizo kubwa linalokabili
sekta ya kilimo na ufugaji nchini kwa wahusika kutozingatia kanuni bora na za
kisasa za kilimo na Ufugaji.
Hivyo katika maonesho haya kuwapo kwa Taasisi
za utafiti zinazozalisha mbegu za kisasa, Kuwapo kwa teknolojia na zana za
kilimo za kisasa ni njia mojawapo ya kuongeza tija kwa jambo ambalo
litawasaidia wananchi kufahamu zaidi kanuni bora za kilimo.
Ufugaji nyuki ni fursa mpya ambayo endapo
Watanzania wataichangamkia itawaletea kipato na kuwaondolea umasikini. Fursa
haihitaji gharama kubwa kuazisha gharama kubwa ni kununua mizinga na kuweka
maeneo rafiki ya nyuki ili waweze kuingia.
Baada ya hatua hiyo hakuna gharama yeyote zaidi
ya kuvuna na kuchakata asali ili iwe na ubora wa kimataifa.
Nyuki wanatoa mazao mengi ikiwa ni pamoja na
nta ambayo inatumika kutengeneza mishumaa na bidhaa nyingine.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment