Tuesday, August 22, 2017

MBUNGE RITTA KABATI AFANIKIWA KUTATUA MGOGORO WA MADEREVA DALADALA WA MANISPAA YA IRINGA NA SUMATRA

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati akiwa anazungumza na madereva daladala wa kituo cha M.Hotel wakati wa kutafuata muafaka wa mgogoro baina madereva na Sumatra Mkoa wa Iringa.
  Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati akiwa anazungumza na madereva daladala wa kituo cha M.Hotel akiwa Sambamba na afisa mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Iringa ngereza pateli katika kituo hicho cha daladala.

Na fredy Mgunda, Iringa

Mbunge wa viti maalumu  mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi CCM amefanikiwa kutatua mgogoro uliotokea jioni hii katika kituo cha daladala cha MR hotel baina ya madereva daladala na Afisa mfawidhi wa Sumatra mkoa wa Iringa gereza pateli.

Kabati alifanikiwa kutatua mgogoro huo wakati akipita katika eneo hilo na kukuta mgogoro ukiwa katika hali isiyokuwa na kawaida ndio aliamua kushuka kwenye gari na kufanikiwa kutatua mgogoro huo.

Akizungumza wakati wa kutatua mgogoro huo mbunge Kabati aliwataka madereva kusitisha mgogoro huo na kukaa mezani kujua tatizo la mgogoro huo nini ndio madereva wakafanikiwa kusitisha mgogoro huo.

"Jamani naombeni mtulie na tuweze kutatua changamoto hiii naombeni chagueni viongozi wenu na twendeni ofisini na viongozi wote wa Sumatra ndio maana unawaona saizi tumekuja kumaliza mgogoro huu"alisema Kabati

Kabati alisema kuwa madereva hao walikuwa wakimlalamikia afisa mfawidhi wa Sumatra ngereza pateli kwa kuendelea kuwanyanyasa madereva wa daladala na kuwaacha huru madereva bajaji kuingilia njia za daladala.

"Walisema kuwa bajaji zimekuwa zikiwapa changamoto nyingi za kuvuruga njia na biashara kudolola kwa jiri ya mfumo huo ili kuweza kutatua changamoto zinazoweza kuzua kitu kingine" alisema Kabati

Kwa upande wao kupitia Mwenyekiti wa madereva daladal kituo cha M.R Hotel, Julias Msanga alisema kuwa imekuwa kawaida kupigwa faini kutokana sababu ambazo hazina kichwa wala miguu hali inayowasababisha kutotimiza hesabu Mara kwa Mara.

Alisema kuwa adhabu hizo zimekuwa zitozwa kwa madereva wa daladala tu lakini madereva bajaji wamekuwa hawatozwi faini hizo kwa kile kinachosemekena wamiliki wa bajaji hizo ni maafisa wa jeshi la polisi.

Akijibu hoja hizo Afisa mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Iringa ngereza pateli alisema kuwa chombo chochote kile kikivunja sheria lazima kichukuliwe sheria kwa mujibu wa Katiba na kanuni za Sumatra.

Ngereza alisema kuwa swala la kusimamia sheria haziangalii kuwa hiki chombo kinamilikiwa na nani na vyombo vyote vya moto vinavyovunja sheria vitachukuliwa hatua.

Lakini baada ya kikao cha takribani masaa mawili baina ya madereva, Afisa mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Iringa ngereza pateli na mbunge Ritta Kabati walifikia muafaka kwa madereva wa daladala kujiwekea sheria ndogo ndogo ambazo hazita sababisha mgogoro tena na kumuomba afisa mfawidhi wa Sumatra Mkoa wa Iringa ngereza pateli kushughulikia swala la bajaji kupakia abiria katika kituo cha M.R Hotel.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More