Ofisi
ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei nchini kwa kipindi cha
Julai mwaka huu umepungua hadi kufikia asilimia 5.2 kutoka asilimia 5.4
iliyokuwapo mwezi Juni mwaka huu hali inayomaanishakasi ya mabadiliko
ya bei za bidhaa imepungua.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za
Jamii, Ephraim Kwesigabo, amesema kupungua kwa mfumuko wa bei wa kipindi
cha Julai mwaka huu kumechangiwa hasa na kupungua kwa baadhi ya bidhaa
za vyakula kwa kipindi kilichoishia Julai 2017 ikilinganishwa na bei za
Juni 2016.
“Baadhi
ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni
pamoja na nyama, kwa asilimia 16.6, bilinganya (10.6), vitunguu (13.2),
karoti (16.9) na viazi mviringo (13.5)" amesema.
Aidha
ameeleza kuwa Shilingi ya Tanzania imezidi kuimarika ambapo uwezo wa
Shilingi 100 katika kununua bidhaa na huduma ulifikia Shilingi 91 na
senti 87 kipindi cha Julai 2017 ikilinganishwa na shilingi 91 na senti
66 ilivyokuwa Juni 2017.
“Mfumuko
wa bei nchini Tanzania una mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi
nyingine za Afrika Mashariki ambapo nchini Kenya mfumuko huo wa Julai
2017 umepungua hadi asilimia 7.47 kutoka asilimia 9.21 Juni 2017 na
nchini Uganda umepungua hadi asilimia 5.70 kwa kipindi cha Julai kutoka
asilimia 6.4 Juni 2017" ameongeza
Hata
hivyo Kwesigabo ameongeza kuwa mfumuko wa bei wa kitaifa unapima
kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote
zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.
0 comments:
Post a Comment