BMG Habari, Pamoja Daima!
Fainali ya
mashindano ya watoto kutoka Vituo vya Huduma ya Mtoto (Compassion) Kanda ya
Mwanza, inatarajiwa kufanyika kesho jumamosi Agosti 26,2017 kwenye uwanja wa
CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mjumbe wa
kamati ya maandalizi, Joram Samwel amesema mashindano hayo yalianza tangu Mei
25 mwaka huu kwa kuhusisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa
pete pamoja na riadha.
Amesema timu
ya soka ya watoto wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18 ya Anglikana Igoma
itachuana na wenzao kutoka Moravian Kigoto kwenye mchezo wa fainali huku timu
ya watoto wenye umri kama huo kutoka AIC Bujora ikichuana na wenzao timu ya PAG
Mabatini ili kumsaka mshindi wa tatu.
Upande wa
timu ya soka ya watoto wenye umri kati ya miaka minane hadi 12 ya EAGT Buzuruga
itacheza wenzao kutoka AIC Buhongwa kwenye mchezo wa fainali huku.
Katika fainali
ya mchezo wa mpira wa pete, timu ya watoto wenye umri kati ya miaka 14 hadi 18
ya Anglikana Igoma,itacheza na wenzao kutoka TAG Nyakato huku wale wenye kati
ya miaka minane hadi 12 kutoka FPCT Pasiansi wakicheza na wenzao kutoka
Moravian Kigoto.
Joram Samwel
amesema lengo la michuano hiyo ni kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto ambapo
wamewasihi wazazi, walezi, watoto pamoja na wapenzi wa michezo Jijini Mwanza, kujitokeza
kwa wingi kuanzia majira ya saa mbili asubuhi ili kushuhudia fainali hiyo
ambayo itakuwa na mvuto wa kipekee.
Tazama video hapo chini
0 comments:
Post a Comment