Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Mhe.Miraji Mtaturu (wa tatu waliokaa), leo Agosti 20,2017 ameongoza uzinduzi wa albamu ya injili ya mwimbaji Elineeema Babu (wa tatu kushoto) uliofanyika kwenye uwanja wa Stendi Mpya ya Ikungi.
Katika uzinduzi huo, Mhe.Mtaturu ameendesha zoezi la uuzaji wa albamu hiyo iitwayo TARATIBU NITAFIKA na kusaidia upatikanaji wa zaidi ya shilingi Milioni Tatu ikiwa ni fedha taslimu pamoja na ahadi.
Mhe.Mtaturu amewahimiza waimbaji wa nyimbo za injili wilayani humo kutumia vyema fursa waliyonayo kwa kuimba nyimbo zenye kuhamasisha amani na upendo nchini, akitolea mfano kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza iliyoimba wimbo uitwao AMANI kwa ajili ya kuhamasisha amani nchini.
Mwimbaji Elineema Babu ameachia albabu ya tatu iitwayo "Taratibu Nitafika" yenye nyimbo nane ambapo amewasihi wadau wengine kumsaidia kwa kununua albamu hiyo (Audio) ili aweze kupata shilingi Milioni Sita zinazohitaji ili aweze kurekodi video ya albamu hiyo. Taratibu Nitafika ni albamu ya tatu baada ya kutanguliwa na albamu mbili ambazo ni Nitumie pamoja na Fanya Kazi ya Bwana.
Mwimbaji Elirehema Babu akitumbuiza kwenye uzinduzi huo hii leo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Mhe.Miraji Mtaturu akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo alikuwa mgeni rasmi
DC Ikungi akizindua albamu hiyo
DC Ikungi akionesha albamu iliyozinduliwa leo
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu (kushoto), akimkabidhi CD Katibu wa CCM wilayani humo (kulia) kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji Elineema Babu
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Mhe.Miraji Mtaturu (kushoto), akimkabidhi CD Baba Askofu wa Jimbo la Singida Dkt.Paul Samweli
BMG Habari
0 comments:
Post a Comment