Tuesday, August 15, 2017

DC ASIA ABDALLAH AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA MTANDAO WA TTCL 4G LTE

 Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizungumza wakati wa uzinduzi wa mitandao wa TTCL 4G LTE katika Mkoa wa Iringa eneo la ofisi za kampuni hiyo.
 Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdallah akizindua huduma ya mtandao wa simu wa TTCL kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa bi Amina Masenza

Na fredy Mgunda, Iringa.

Watanzania wametakiwa kuanza kuutumia mtandao wa simu wa TTCL kwa kuwa umeboreshwa kwa kiwango kikubwa na huduma zao zinazingatia wateja wake ili kuendelea kiinufaisha serikali kwa kuwa mtandao huo unamilikiwa na serikali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa TTCL 4G mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alisema kuwa wananchi wanapaswa kuunga mkono mtandao huu wa kizalendo ambao unahuduma nyingi nzuri.

“Ukiangalia utagundua kuwa mtandao wa TTCL inahuduma ya pesa ambazo zina makato madogo sana kulinganisha mitandao mingine hivyo nawasiii wananchi wa mkoa wa iringa kuanza kutumia huduma za mtandao huu wa kizalendo” alisema Abdallah

Abdallah aliwataka wananchi kuanza kuvithamini vitu vya wazawa kwanza ili kuleta maendeleo ya maendeleo kwenye kampuni na taasisi za kizalendo  ndio maana mkuu wa mkoa wa Iringa na wakuu wa wilaya wote wa mkoa huu wameamua kujiunga na mtandao huu wa TTCL.

“Mimi,mkuu wa mkoa ,mkuu wa wilaya Richard Kasesela  na viongozi wengine wamejiunga na mtandao huu wa TTCL 4G ambao unakasi kubwa kwenye upande wa internet na huduma nyingine ziboreshwa na zimekuwa bora sana” alisema Abdallah

Aidha Abdallah alisema kuwa kampuni hii ya kizalendo imekuwa ikihudumia jamii kwa njia tofautitofauti za kimaendeleo hasa kwa kuunga mkono kwenye michezo mbalimbali hapa nchini.

“Kama unakumbuka hivi karibuni kulikuwa na mshindano ya Ritta kabati challenge cup ambapo kampuni hii ya kizalendo ilichangia zaidi ya milioni mbili kufanikisha kuendesha mashindano hayo hivyo utagundua kuwa TTCL imekuwa ikirudisha faida kwa wananchi”alisema Abdallah

Abdallah alisema kuwa TTCL wana bando kuwa kwa gharama nafuu hivyo naomba wananchi wanaopenda kutumia mitandao ya kijamii wanapaswa kujiunda na mtandao huu kwa kuwa unagharama nafuu na internet yake inakasi nzuri kulingana na mitandao mingine.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya TTCL nchini Waziri Kandamba alisema kuwa TTCL imekuja kuboresha maisha ya watanzania wanaopenda kutmia mitandao ya simu kwa kuwa wamejipanga kufanya kazi kishindani tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

“Leo tumefanya uzinduzi wa mtandao wenye kasi kubwa 4G LTE ambao utakuwa unakata kiu kwa wanaopenda kutumia mitandao ya kijamii kwa kuwa tumeboresha huduma zetu zote katika mtandao huu” alisema kandamba

Kandamba aliwataka watanzania kuvitumia na kuvithamini vitu vya kwao kama makampuni ya wazao  ndio maana TTCL ilirudi kuwatumikia watanzania kwa kuboresha huduma zetu zote.

“Wewe jaribu kutumia mtandao wetu wa TTCL utapata jibu zuri kwa kiasi gani tumeboresha huduma hii ambayo watanzania wengi waliikosa kwa muda mrefu hivyo nawaomba watanzania kujiunga na mtandao wetu wa TTCL wenye huduma bora” alisema Kandamba

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More