Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe
amewataka Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya nchini kuanzisha mfuko wa
wasanii kwa lengo la kutatua changamoto ya udhamini inayowakabili.
Ameyasema
hayo Jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na Wasanii hao ambacho
kilijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili na namna ya kukabiliana
nazo hivyo kuwataka kutokata tamaa
Amesema
kuwa kutokana na malalamiko na changamoto mbalimbali zinazowakabili
Wasanii, ambazo nyingi zinasababishwa na mikataba inayowanyonya Wasanii
katika kazi zao, ni vema sasa Wasanii hao kupitia Chama chao cha
Tanzania Urban Music Association (TUMA) kuanzisha mfuko ambao utakua
unatoa mikopo kwa Wasanii ili kuwezesha utendaji wa kazi zao pasipo
kutegemea wadhamini.
“Ninafikiri
dawa tunayohitaji ni kuanzishe mfuko wa Wasanii ambapo kila Msanii
atatakiwa kuchangia fedha. Jambo ambalo litawavutia wadau wengine
kuchangia mfuko huo na kuwaondoa katika dhana ya utumwa, na mfuko huo
utamsaidia msanii aliyejisajili kupata mkopo bila kutozwa riba yoyote,” alielezea Waziri Mwakyembe.
Aidha,
Mwakyembe amesema kuwa Tasnia ya Sanaa ina mchango mkubwa katika
kuongeza pato taifa hivyo ametaka tasnia hiyo kurasimishwa ili kupunguza
tatizo la ajira na pia kutumika kama chombo maalumu cha kuielimisha
jamii kwani kupitia Sanaa wananchi hupata ujumbe kwa urahisi.
Hata
hivyo, Mwakyembe ameunda Kamati ya kushughulikia masuala yanayowakabili
Wasanii ikiwemo sera na sheria ili kuboresha maslahi ya Msanii. Wasanii
wanaounda Kamati hiyo ni Azma Mponda, Niki wa Pili pamoja na Witness
Mwaijanga.
Kwa
upande wake Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Onesmo Kayanda amesema
kuwa, ili kuboresha na kukuza tasnia ya muziki nchini ni lazima kuwepo
na soko la uhakika la kazi hizo pamoja na tuzo mbalimbali ambazo
zitatumika kutia hamasa kwa wasanii.
0 comments:
Post a Comment