Mwenyekiti wa timu hiyo Dickson Nathan Lutevele maalufu kwa jina la Villa akizungumza na waandishi wa habari katika studio za uzalishaji vipindi za Ebony fm Iringa
Na fredy Mgunda, Iringa
Viongozi wa timu ya Mpira ya Mufindi united zamani kurugezi Fc wameomba wadau na wapenda mpira Mkoani Iringa kuichangia timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza mwaka wa 2017/2018 ili iweze kufanikiwa kuingia ligi kuu msimu ujao.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa timu hiyo Dickson Nathan Lutevele maalufu kama kwa jina la Villa alisema kuwa lengo la kamati ya timu nikuhakikisha msimu huu timu inapanda kutoka daraja la kwanza hadi ligi kuu ndio maana timu tumeirudisha kwa wananchi.
"Tukuwa ligi daraja la kwanza kwa takribani miaka mitano sasa hatujawahi kupanda ndio maana mwaka huu tumeamua kubadilisha jina timu na kuirudisha kwa wananchi ili kuwa karibu na kuweza kuisaidia katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo ya timu hivyo naomba wananchi waipokee hii timu kama ya kwao" alisema Villa
Aidha Villa aliongeza kuwa timu ya Mufindi united inatakuwa inachezea mechi zake katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora masheli uliopo katika Manispaa ya Iringa hivyo anaomba wadau wa soka mkoa wote wa Iringa kuanza kuiunga mkono timu ili kupata timu mbili zitakazo kuwa ligi kuu.
"Miaka yote timu imekuwa ikichezea uwanja wa wambi kama uwanja wa nyumbani lakini msimu huu tumebadili jina la timu na tumebadili uwanja pia hivyo tunategemea mabadiliko makubwa sana na matokeo yake tupande ligi juu"alisema Villa
Kwa upande wake Katibu wa timu ya Mufindi united Rugatekanisa Isidory aliviomba vyombo vya habari kuwasaidia kufikisha kikamilifu habari za timu hiyo kwa kuwa sasa ipo mikononi kwa wananchi wa Mufindi na mkoa mzima wa Iringa.
"Nyie waandishi wa habari unaushawishi mkubwa sana kwa wananchi na wadau wa Mpira wa miguu hivyo tunaomba msaada wenu kufikisha kilio chetu kwa wananchi na wadau wa Mpira wa Mkoa wa Iringa waliopo ndani na nje ya Mkoa" alisema Isidory
0 comments:
Post a Comment