Thursday, August 3, 2017

ASKOFU SOLOMONI MASANGWA AMUONYA MBUNGE WA CHADEMA

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT ) kanda ya kaskazini kati,Solomoni Masangwa,amemwonya mbunge wa Siha,Godwin Mollel (CHADEMA)kuacha kuhubiri siasa chonganishi kanisani kwa kuwatukana viongozi waliopo madarakani waliochanguliwa na wananchi.

Kauli hiyo ameitoa jana wakati wa hafla ya uzinduzi wa kanisa KKKT dayosisi ya kaskazini kati,jimbo la Arusha Magharibi, usharika wa Kiranyi ,wilaya ya Arumeru,ambapo askofu huyo alikerwa na hatua ya mbunge Mollel kujinadi kisiasa huku akimshambulia rais John Magufuli bila kujali kuwa mkusanyiko uliopo kanisani ni waumini wenye itikadi tofauti za kisiasa na kwamba mahala pale palikuwa sehemu takatifu ya kuabudia.

‘’Katika kanisa nisinge penda kuona siasa ikihubiriwa hapa, mh.mbunge wa siha amesema kuwa kuna mwanaume mmoja hapa Tanzania anajiona yeye ni kidume kuliko wanaume wote ila ajue wapo wanaume zaidi yake sasa sijui anamlenga nani bila shaka ana maanisha raisi Magufuli kauli hiyo sio njema sana na inasitahili kukemewa na kila mtu ‘’alisema Askofu

Source: jamii forum

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More