Thursday, August 24, 2017

DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA

 Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la chanzo cha mradi huu wa maji katika mji mdogo waIlula
 Mkuu wa mkoa wa iringa Amina masenza akifurahia kufika kwenye chanzo cha maji pamoja na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kwa kuwa wanajua hilo ndio litakuwa suluhisho la mda mrefu kwa wakazi wa mji mdogo wa Ilula
viongozi wa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa wakiwa wanaelekea kwenye chanzo cha maji kwa ajili ya kujua jinsi gani kitaweza kutatua kero za wananchi wa mji wa mafinga
 mjumbewa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa ndugu mosha akiwa njiani kuelekea kukikagua chanzo hicho cha maji
 katibu msaidizi wa chama cha mapinduzi mkoani iringa akiwa sambasamba na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalla wakielekea kukagua chanzo kipya cha maji kwa ajili ya wananchi wa mji mdogo wa mafinga


Na Fredy Mgunda,Iringa

Halmashauri ya wilaya ya kilolo inatarajia kutatua kero ya maji iliyodumu kwa miaka mingi katika mji mdogo wa Ilula mkoani Iringa kwa kutenga kiasi cha dola za kimarekani 9,548,827 kwa ajili ya kujenga chanzo kipya cha maji yatakayo weza kutatua changamoto hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekeleza wa ilani ya chama cha mapinduzi  wilayani kilolo mkuu wa mkoa wa iringa ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya siasa ya mkoa bi Amina Masenza alisema kuwa wameamua kutafuta chanzo kipya ili kutatua tatizo la maji katika mji mdogo wa Ilula.

“Leo nimefika hadi huku kwenye chanzo cha maji ambacho naamini kuwa kitafanikiwa kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula hivyo lazima waisimamie ipasavyo ilani ya chama na kuhakikisha kuwa wanatatua  matatizo ya wananchi”alisema Masenza

Aidha Masenza alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muuungano wa Tanzania dr John Pombe Maguli kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alivitaja baadhi ya vyanzo ya maji na uwezo wa uzalishaji ambavyo vinatoa huduma kwa mji mdogo wa Ilula ni Ilomba kutoka kijiji cha Imalutwa na Idemule kutoka kijiji cha Mazombe kwa ujumla vinazalisha wastani wa uzalishaji wa maji wa mita za ujazo 1,142 kwa siku.

Abdallah alisema kuwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula unamahitaji makubwa ya matumizi ya maji ambapo kwa siku wanahitaji maji ya mita za ujazo 2687 kwa siku hivyo hadi sasa kunaupungufu wa mita za ujazo 1545 kwa siku.

“Mji huu unakuwa kwa kasi kubwa hivyo matumizi ya maji yamekuwa makubwa mno ndio maana tumeanza  kujenga chanzo kingine ambacho kitakuwa na suluhisho kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula na kutaua kabisa tatizo la maji” alisema Abdallah 

Abdallah aliwataka wananchi na viongozi wa ngazi zote kuacha tabia ya kuharibu vyazo vya maji na mazingira kwa ujumla hivyo atakaye kamatwa anafanya uhalibifu wowote ule sheria itachukua mkondo wake.

“Ni malufuku kwa wakulima kulima kwenye vyanzo vya maji,wafugaji kufujia mifugo kwenye vyanzo vya maji pamoja na ukaji wa miti hovyo hapo nitakuwa mkali sana kwa watu ambao watakiuka haya nayoyasema hii leo kwa kuwa kila kitu kipo kisheria “ alisema Abdallah

Naye meneja wa mamlaka ya maji wa mji mdogo wa Ilula Enock Ngoyinde aliiomba serikali ya na kamati ya siasa ya mkoa wa iringa kusaidia upatikanaji wa pesa kwa wakati za kumaliza mradi huu wa maji ili wananchi waanze kupata huduma bora mapema iwezekanavyo.

Ngoyinde alisema kuwa mradi huo ukikamilika utakuwa umeongeza eneo la utoaji wa huduma vya maji kutoka wastani wa asilimia 62 hadi asilimia 75 na kuwahudumia wananchi zaidi ya elfu ishirini na tano (25000) ambao watakuwa na mtandao wa bomba za maji.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More