Thursday, January 12, 2017

WAKAZI WA MIJINI WAHIMIZWA KUJIKTA KWENYE BUSTANI ZA MAKOPO NA MIFUKO.

#LakeFm Habari
Wakazi wanaoishi maeneo ya mijini nchini wamehimizwa kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga kwa kutumia masalia ya makopo na mifuko ya aina mbalimbali ili kuondokana na uchafunzi wa mazingira.

Mwanamama Victoria Buzare ambaye ni mjasiriamali kutoka Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, ameyasema hayo wakati akizungumza na Lake Fm huku akiongeza kwamba kilimo hicho pia kinawaepusha wanajamii na athari za kutumia mbogamboga zenye kemikali.

Amesema kilimo hicho kinagharimu mtaji kidogo hadi shilingi 5,000 ambazo mkulima anaweza kulima aina tatu za mbogamboga ikiwemo sukumawiki, nyanya chungu, biringanya na nyinginezo.

Buzare amewashauri wanafamilia wote wanaoishi mijini kuhakikisha wanakuwa na bustani za makopo na mifuko kwani ni salama kwa matumizi ya chakula na pia rahisi kusimamia ikizingatiwa ndoo moja ya maji kwa siku inatosheleza mahitaji yake.
Kwa maoni na ushauri ama swali, wasiliana na Victoria Buzare (pichani) kwa nambari za simu 0754 21 85 55.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More