Na. Tundu Lissu
Waheshimiwa
na makamanda poleni kwa mapambano na hongereni kwa kazi kubwa
mliyoifanya kwenye chaguzi hizi. Naona kila mmoja wetu anasikitika jinsi
matokeo ambavyo yamekuwa tofauti na matarajio yetu na kazi
tuliyoifanya.
Ni
rahisi, katika mazingira haya ya kushindwa na kabla vumbi halijaisha,
kuanza kulalamika, kunyoosheana vidole na kukatishana tamaa. Hii
haitusaidii sana. Badala yake, tunachohitaji zaidi ni ‘brainstorming’
kuliko ‘blamestorming.’ Naomba nifanye ya kwanza. Chaguzi ndogo za
ubunge au udiwani ni ngumu sana kushinda katika mazingira halisi ya nchi
yetu.
Mifano
michache inathibitisha ukweli huu. Katika election cycle ya ’05-’10,
tulishinda Jimbo la Tarime lakini tukapigwa Biharamulo Magharibi na
Busanda. Tarime lilikuwa Jimbo letu tangu Uchaguzi Mkuu wa ’05, Busanda
lilikuwa la maCCM na Biharamulo Magharibi lilikuwa la TLP. Sikumbuki
vizuri kama tulishinda Kata hata moja katika mzunguko wa uchaguzi wa
kipindi hicho.
Katika
election cycle ya ’10-’15, tulipigwa Igunga licha ya kazi kubwa
tuliyofanya, lakini tukashinda Arumeru Mashariki iliyokuwa chini ya
maCCM. Vile vile tulishindwa Kalenga, Chalinze na Ulanga Magharibi
yaliyokuwa ya maCCM tangu Uchaguzi Mkuu wa ’10.
Kwenye
chaguzi za Kata za ’12 kama mnakumbuka, licha ya kazi kubwa na
rasilimali nyingi, tulipata Kata tatu tu kati ya 26 zilizokuwa
zinagombaniwa. Ukiachia Ifakara Mjini ya Mh. Juakali, Kata nyingine
mbili – Kiboriloni na Iseke – zilikuwa zetu tangu Uchaguzi Mkuu wa ’10.
Kwa
mantiki hii, matokeo ya jana sio ya kushangaza sana. Kata ya Duru
ilikuwa ya kwetu na tumeitetea, nyingine zote tulikopigwa zilikuwa za
maCCM. Hatujanyang’anywa iliyokuwa yetu, hatujanyakua zilizokuwa zao.
Hata hivyo, funzo kubwa zaidi la historia ya chaguzi hizi ni hili hapa:
licha ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo hizi, tumeendelea kufanya vizuri
zaidi katika kila Uchaguzi Mkuu uliofuatia kipigo cha chaguzi ndogo.
Mwaka
’10 tulifanya vizuri zaidi licha ya kupigwa Busanda na Biharamulo
Magharibi katika mzunguko wa ’05-’10. In fact, tulichukua Jimbo la
Biharamulo Magharibi mwaka huo. Na tulipata Kata nyingi zaidi ’10 kuliko
ilivyokuwa ’05. Mwaka ’15 tulipata ushindi mkubwa zaidi katika Kata na
majimbo licha ya kupigwa kwenye chaguzi ndogo za mzunguko wa ’10-’15.
Hoja
yangu hapa ni kwamba uchaguzi wa marudio hauna direct and negative
bearing kwenye matokeo yetu ya Uchaguzi Mkuu unaofuatia. On the
contrary, uchaguzi wa marudio unatupa fursa ya kupanda mbegu ambayo,
ikitunzwa vizuri, inakuwa na mazao bora kwenye chaguzi zinazofuatia.
Kwa
upande mwingine, chaguzi za marudio – kwa sababu ya udogo au uchache wa
maeneo yanayogombaniwa – yanawapa maCCM fursa ya kutumia nguvu kubwa za
rasilimali na za kidola ukilinganisha na tunazotumia sisi. Kwenye
Uchaguzi Mkuu unaofuatia, nguvu hizo zinasambazwa nchi nzima na kwa hiyo
effectiveness yake inapungua.
Ndio
maana tumefanya vizuri zaidi kwenye Uchaguzi Mkuu kuliko kwenye chaguzi
ndogo za marudio. Hili, kwa maoni yangu, ndilo fundisho kuu la chaguzi
hizi za marudio. Hatuna sababu kubwa ya kushangilia kutokana na matokeo
ya jana. Hata hivyo, hatuna sababu yoyote ya kuomboleza pia. Obviously,
maCCM na wapambe wao wataandika ‘wasifu wa marehemu’ wa CHADEMA/UKAWA na
kuutangaza dunia nzima na kwa sauti kubwa. Hilo lisitupofushe macho
yetu, hata kama linakera sana.
0 comments:
Post a Comment