Friday, January 27, 2017

WAKULIMA WATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA YENYE TIJA ,ILI KUPATA MAZAO YENYE BORA

 mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho ya zana za kilimo  katika viwanja  vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani 
 Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike   akimuelewesha mkulima jinsi kampuni yao inavyofanya kazi ya kusambaza teknolojia ya umwagiliaji wa Matonye
 Washiriki ambao ni wakulima wakifuatilia kwa makini mada ambazo zilikuwa zikiendelea wakati wa ufunguzi

   Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo  ufugaji holela , ambao  hupelekea uharibifu wa mazingira,Teknolojia duni pamoja na ugumu wa kupata mitaji ya kuboresha miundombinu ya kilimo.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro,wakati akiofungua Maonyesho ya zana za kilimo  katika viwanja  vya Taasisi ya Utafiti wa kilimo ya Seliani  vilivyopo ndani ya jijini Arusha ambapo ni mara ya kwanza kufanyika  .

Alisema kuwa sekta ya kilimo inakabiliwa na changamoto za ufugaji holela ambao unasababishwa na wafugaji ,wakulima kutumia teknolojia duni au zazamani katika ukulima  pamoja na wakulima wengi kukosa mitaji ya kubesha miundo mbinu ya kilimo

Alisema kuwa hii inachangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha maendeleo ya sekta hii kutokana na wananchi wengi kutumia kilimo cha kawaida badala yakutumia kilimo cha kisasa ambacho kinaleta tija .

“hapa Tanzania zaidi ya asilimia 75% wanategemea kilimo lakini kati yao n asilimia 1.5 tu ndio wanatumia kilimo  cha kisasa kama kilimo cha umwagiliaji ,kupanda mbegu  bora  pamoja na kilimo cha matone hivyo ni vizuri wakulima wetu kujitaidi kutumia kilimo cha kisasa ili kuweza kufanya kilimo chenye tija ambacho kinamnufaisha yeye mkulima mwenyewe na kuachana na kilimo cha kawaida au naweza sema cha kienyeji”alisema Daqarro

Alisema kuwa watanzania tunauwezo wa kuzalisha  mazao bora kwakuwa tuna aridhi nzuri ,maji mengi ya kutosha tunayo kwani tunamito mingi inayotoa maji  hivyo tukiamua kuwekeza na kulima kilimo chakisasa tunaweza kusaidika na hata   pato la mkulima litakuwa na sio mkulima tu na pia pato la serikali pia litaongezeka kutokana na kilimo.




Aidha mkuu huyo wilaya alisea kuwa serikali inawashukuru wadau kwa kuupa mkoa wa Arusha heshima ya kufanyika kwa maonyesho hayo ambayo yatafanyika kwa muda wa siku mbili hivyo amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika kujifunza teknolojia mpya za kilimo na ubunifu wautaalamu mbalimbali .



“napenda pia kuwataka  waonyeshaji kuangalia suala la bei kwani  asilimia 75-80 ya wakulima ni wakulima wadogowadogo hivyo ni vyema wakauza bidhaa zao kwa bei nafuu ili wakulima wa hali ya chini aweze kumudu kununua bidhaa ili waweze kuendana na kasi ya kilimo cha kisasa ,Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo wanaangalia ni kwa namna gani
wataweza kuboresha sekta hii ya kilimo kwa kutoa elimu mbalimbali kwa wakulima ili kuepukana na kilimo duni ambacho kinasababisha hasara kwa wakulima nchini”alisema Daqorro




Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani Dr Daniel Mafuru   amesema kuwa wamekua wakishirikiana na wadau mbalimbali wa kilimo ,katika uzalishaji wa Teknolojia ,pamoja na kuwatafutia wadau wa kilimo masoko ya mazao yao.

Aidha alisema kuwa  Seliani wapo  tayari kuwaunganisha wakulima na waonyeshaji wa teknologi ,ilikuwawezesha wakulima kupata mafunzo na kubadilishana ujuzi  pia iwapo watauwaunganisha itawasaidia  kufahamu namna ya kuhifadhi mazao yao baada ya uvunaji ili wasipoteze mazao kama ilivyokuwa kabla ya kupata elimu hiyo ya kilimo.

 Kwa meneja masoko wa kampuni ya John Deere ambaye pia ndio wadhamini wakuu wa maonyesho haya Wayne Travas alisema kuwa kampuni yao  zinatefaya kazi ya kuwaletea wakulima wadogo mashine za kilimo ambazo zitawasaidia kufanya kazi vizuri  na kwa teknologia za kisasa pamoja na ubora mwingi.


 mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti ya Seliani Dr Daniel Mafuru   Akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo
 Washiriki wakifuatilia

 meneja masoko wa kampuni ya John Deere ambaye pia ndio wadhamini wakuu wa maonyesho haya Wayne Travas Akifafanua jambo  mbele ya waandishi wa habari
 katika maonyesho haya pia kamera yetu  iliweza kumkuta mwimbaji mashuhuri wa jijini hapa Nakaya Sumari akiwa na Phidesia Mwakitalima nao pia waliuthuria  katika maonyesho hayo ili nao waweze kulima kilimo chenye tija
 Baaadhi ya wakulima wakiangalia matrekta ya kisasa yanayouzwa na kampuni ya John Deere nambao ni wathamini wakuu

 Mmoja wa mkulima akiangalia jinsi ngowe zilizolimwa kwa njia ya matone zilivyostawi shambani
 Afisa mauzo wa kampuni ya Irrico Saimoni Manyike akiwaonyesha wakulima hawapo pichani jinsi  kilimo cha umwagiliaji wa mtone kinavyokuwa


Mshauri wa sekta ya kilimo na ufugaji  David Nyange akifafanua jambo katika uzinduzi wa maonyesho hayo


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More