Tuesday, January 24, 2017

KAMATI YA TAIFA YA MATUMIZI YA BIOTEKNOLOJIA SALAMA YARIDHISHWA NA UTAFITI WA MAHINDI KATIKA KITUO CHA MAKUTUPORA MKOANI DODOMA

Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), waandishi wa habari na watafiti wakielekea ukumbuni walipowasili Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Kanda ya Kati Makutupora mkoani Dodoma leo asubuhi kuangalia shamba la majaribio la mahindi yaliyotokana na teknolojia ya uhandisi jeni (GMO)
 Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour akizungumza katika mkutano huo wakati akiwakaribisha wajumbe wa NBC katika kituo hicho cha utafiti wa kilimo cha Makutupora cha mkoani Dodoma.
Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kkushoto), akitoa maelezo mafupi kwa wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), kabla ya kuingia katika shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo.
Waandishi wa habari, Lucy Ngowi wa gazeti la Habari Leo (kushoto), Dotto Mwaibale wa Jambo Leo (katikati) na Fatma Abdu wa Daily News wakijadiliana jambo katika shamba hilo la majaribio.
Mwonekano wa shamba hilo.
Mjumbe wa Kamati hiyo, Mhandisi Kissina kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, akiangalia hindi lililotokana na teknolojia hiyo.
Mshauri wa mradi wa Wema, Dk. Alois Kullaya (kulia), akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC), kuhusu matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) walipotembelea shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo.
Meneja wa shamba hilo, Bakar Mohamed akielezea kuhusu 
shamba hilo.

Safari ya kuelekea kuangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti ikiendelea.
Wajumbe wa kamati hiyo na watafiti wa kilimo wakiangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti huo.
Wajumbe wa kamati hiyo na watafiti wa kilimo wakiangalia shimo la kuchomea uchafu mbalimbali baada ya kufanya utafiti huo.
Mlinzi wa shamba hilo, Mbisi Masinga akiwa kazini.
Watafiti wa Kilimo na Wajumbe wa Kamati ya NBC wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya shamba hilo.


Na Dotto Mwaibale, Dodoma

KAMATI ya Taifa ya Matumizi Salama ya Bioteknolojia (NBC) imeridhishwa na  matumizi ya Teknolojia ya Uhandisi Jeni (GMO) yenye lengo la kuwakwamua wakulima nchini.

Wajumbe wa kamati hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari wakati walipotembelea shamba la majaribio la mahindi yaliyoboreshwa kwa kutumia Teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) chini ya mradi wa Wema katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Makutupora mjini Dodoma leo walisema hatua iliyofikiwa na watafiti hao ni kubwa hivyo haipaswi kuachwa ikapotea bure. 

Elisa Moses kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe ambaye ni mjumbe wa NBC alisema teknolojia hii ya bioteknolojia ni nzuri na inaonesha uhalisia halisi na inaweza kusaidia changamoto za ukosefu wa chakula iliyopo nchi.

"Binafsi nimefurahi kujionea hali halisi ya teknolojia hii hasa ninapoyaona mahindi haya ya GMO yalivyomakubwa kwani ni muhimu sana katika kukabiliana na ukame uliopo sehemu kubwa nchini" alisema Moses.

Mjumbe mwingine wa kamati hiyo kutoka Chemba ya Wanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo, Magdalene Mkocha alisema wamefurahi kuona jambo walilolipitisha linafanyiwa kazi vizuri na linaleta matumaini makubwa kutokana na matokeo ya jaribio hilo.

Alisema wadau wa sekta binafsi wanasubiri kwa hamu kuhusu matokeo hayo baada ya kuthibitishwa na takwimu za kisayansi kwani kwa kuangalia kwa macho mahindi yanaonekana ni bora zaidi.

Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Kanda ya Kati Dodoma, Sebastian Kandira alisema hapo awali tafiti hizo zilikuwa hazifikishwi kwa wakulima ndio maana zilikuwa hazieleweki vizuri lakini hivi sasa wameanza kuzielewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo Kanda ya Kati, Leon Mroso alisema wakati wanaanza majaribio hayo kulikuwa na changamoto nyingi kutokana na wadau kutokuwa na uelewa hasa kwa mahindi yaliyobadilishwa vinasaba kikubwa ni mshukuru Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba  kwa kufika katika shamba hili la majaribio ambalo tulipanda mahindi Oktoba 5, mwaka jana na kutupa faraja kuwa kuna kila sababu ya kuharakisha matumizi ya teknolojia hiyo ili iweze kutumika kama zinazofanya nchi zingine zinazofanya tafiti za namna hiyo.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More