Tuesday, January 24, 2017

CCM YASHINDA VITI VYA UDIWANI MUFINDI

Msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ametangaza matokeo ya uchaguzi mdogo wa kata mbili za Ikweha na Igombavanu zote zikiwa jimbo pacha la Mufindi kaskazini, ambapo matokea yanaonesha kuwa chama cha mapinduzi CCM kimefanikiwa kutetea viti vyote viwili katika kata hizo.

Taarifa ya msimamizi wa uchaguzi kupitia kitengo cha habari na mawasilino cha halmshauri ya wilaya ya Mufindi, zinaonesha kuwa, katika kata ya Ikweha jumla ya watu waliokuwa mejiandikisha kupiga kura walikuwa elfu 03 mianane 11, (3811) waliojitokeza kupiga kura ni elfu 02 miatatu na 07, (2307) ambapo mgombea wa CCM Bw.Albeto Chaula amepata kura elfumoja mianne na 05 (1405) sawa na asilimia 61% mgombea wa CDM Bw Ayubu Masika amepta kura mianane na 77(877) sawa na asilimia 38% huku mgombea wa CUF Bw. Meshack Manga akipata kura 25 sawa na asilimia 1%.

Taarifa hiyo imeainisha pia matokeo ya kata ya Igombavanu, ambapo waliojiandikisha kupiga kura walikuwa elfu 03 miambili 83 (3283) wakati kura zilizopigwa zilikuwa elfu 02 na 27(2027) kati ya hizo mgombea wa CCM Bw. Rashid Mkuvasa wamejikusanyia kura elfu moja miambili 83 (1283) sawa na asilimia 63% huku mgombea wa CDM Bw.Scholar Mitimingi amepata kura miasaba na 44( 744) sawa na asilimia 37%.

 Katika uchaguzi huo jumla ya kura 64 zimekataliwa  ambapo Ikweha ni kura 36 na Igombavanu kura 28. Aidha, zoezi la uchaguzi katika kata zote mbili lilikuwa la amani na utulivu.

Uchaguzi wa kata hizo, uliitishwa na tume ya taifa ya uchaguzi baada ya kufariki kwa waliokuwa madiewani wa kata hizo mbili kupitia chama cha mapinduzi CCM ikiwa ni miezi michache baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More